KAMATI ya Kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam jana na kupitia majina ya wanamichezo waliopendekezwa kuwania tuzo hizo.
Usiku wa Tuzo utafanyika Desemba 12 mwaka huu ukumbi wa Diamond, Jubilee (VIP), Dar es Salaam, ambapo wanamichezo mbalimbali waliofanya vizuri kati ya Juni 2013 hadi Juni 2014 watakabidhiwa tuzo zao.
Ni imani yetu kwamba zaidi ya wanamichezo 40 watakabidhiwa tuzo zao siku hiyo, ambapo kamati imejiridhisha kwamba wanaowania tuzo hiyo wanastahili kulingana na mapendekezo ya vyama vya michezo kupitia Kamati zao za Ufundi.
Mshindi wa kila tuzo ataingia katika mchakato wa kumpata Mwanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2013/2014, ambapo pia siku hiyo ya sherehe za tuzo itatangazwa zawadi ya Tuzo ya Heshima kwa yule ambaye itaonekana alikuwa na mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya kimichezo hapa nchini. Tuzo hizo ni kuanzia Juni 2013 hadi Juni 2014.
ORODHA KAMILI YA WANAOWANIA TUZO ZA TASWA 2013/2014
OLIMPIKI MAALUM:
Wanaume: Raphael Kalukula, Pazi Mwinyimkuu na Hatibu Matali
wanawake: Blandina Blasi, Shida Jaha na Mwanaharusi Risasi.
MPIRA WA KIKAPU;
Wanaume:Lusajo Samwel (Oilers), Erick Mchemba (ABC)
wanawake:Sajda Ahmed Lyamaiga(Don Bosco Lioness), Rehema Silomba (Don Bosco Lioness) na Orlyn Titus (Don Bosco Lioness).
MPIRA WA MAGONGO;
Wanaume:Yohana Wilson, Focus Paul, Deep Vaja
Wanawake: Valentina Quarantta, Kidawa Seremala na Mary Mhina
MPIRA WA WAVU:
Wanawake: Yasinta Remmy (Jeshi Stars), Hellena Richard (Magereza) na Teddy Abwao (Jeshi Stars).
WanaumE: Kelvin Peter Severino (Magereza), Nassoro Sharifu (Jeshi Stars) na Athuman Rupia (Jeshi Stars).
RIADHA:
Wanawake: Zakia Mrisho, Jaqueline Sakilu na Catherine Lange
Wanaume:Alphonce Felix, Dickson Marwa na Fabian Nelson.
BAISKELI:
Wanawake: Salome Donald, Martha Anthon na Sophia Adson.
Wanaume: Richard Laizer, Hamisi Mskala na Gerald Konda,
GOFU:
Wanaume:Nuru Mollel, Abasi Adam na Frank Mwinuka
Wanawake: Madina Iddi, Hawa Wanyeche na Angel Eaton
GOFU YA KULIPWA:
Hassan Kadio, Yassin Salehe na Geoffrey Leverian
JUDO
Wanaume: KOMBO Masoud Amour, MBAROUK MbaroukSleiman
Wanawake: Grace Alfonce Mhanga, Salma Omari Othman.
TENISI WALEMAVU:
Wanaume; Novatus Emmanuel Temba, Yohana Assa Mwila, Juma Mohamed Hamisi
Wanawake; Rehema Selemani Saidi,Bihawa Mustafa Ituji
TENISI:
Wanaume: Tumaini Martin, Emmanuel Malya na Omari Sulle
Wanawake: Rehema Athumani, Edna John, Georgina Kaindoh
NETIBOLi:
Doritha Mbunda (JKT Mbweni), Berina Kazinja (Magereza Moro), Andressa Andrea (Magereza Moro)
Ngumi za Ridhaa: Fabian Gaudence, Ahmed Furahisha na Ally Abdul Ahmed
SOKA;
Wanawake:
Sophia Mwasikili, Sherida Boniface na Amina Ally
WANAUME
Elias Maguli (Ruvu Shooting-sasa Simba), Erasto Nyoni (Azam FC) na Nadir Haroub (Yanga).
WACHEZAJI WA NJE WANAOCHEZA TANZANIA
Kipre Tchetche (Azam), Amis Tambwe (Simba) na Mbuyu Twite (Yanga).
WATANZANIA WANAOCHEZA NJE
Richard Laizer (baiskeli-Afrika Kusini/Uswisi)
Mbwana Sammata (TP Mazembe-soka DRC), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe-soka DRC).
NGUMI KULIPWA, Francis Cheka, Ramadhani Shauri na Said Mbelwa.
MPIRA WA MIKONO
Wanaume: Hemedi Salehe (JKT), Msafiri Makoti (Ngome) na Abinery Kusena (JKT)
Wanawake: Veronica Mapunda, Subira Omary na Mwajabu Lugato
WANAMICHEZO CHIPUKIZI
Omari Sulle (tenisi)
Sheridah Boniface (soka wanawake)
Aishi Manula (soka wanaume-Azam)
MWANAMICHEZO BORA WA MWAKA 2013/2014: ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA KATEGORI.
TUZO YA HESHIMA:
Itatangazwa ukumbini siku ya sherehe Desemba 12 mwaka huu.
Rehure Nyaulawa
Mwenyekiti Kamati ya Tuzo
03/12/2014