DAWASCO inaomba radhi wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kwa kukosekana kwa huduma ya Maji kutoka katika mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini kwa wastani wa saa 72 kwa siku za Ijumaa hadi Jumatatu ya tarehe 28, 29 na 30 November 2014.
Kukosekana kwa huduma hii kulitokana na kazi ya mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (cross-connection) katika mtambo wa Ruvu Chini eneo la Mpiji, Bagamoyo na eneo la Chuo Kikuu Ardhi (Makongo Juu).
Tunapenda kuwajulisha wateja wetu na wananchi kwa ujumla kuwa huduma ya Maji imerejea na mtambo wa Ruvu Chini umewashwa tarehe 2/12/2014 saa tano asubuhi.
Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kulisababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji;
Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe.
Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.
Kumbuka kulipia huduma ya Maji unayotumia kila Mwezi.
Imetolewa na ofisi ya uhusiano, Dawasco - Makao Makuu.