Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akiagana na Balozi wa Australia nchini anayemaliza muda wake, Geoff Tooth.
Balozi Geoff Tooth (kulia) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Ngosi Mwihava ambapo Balozi huyo alimshukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka katika Wizara na kumhakikishia kuwa Serikali ya Australia imedhamiria kuuenzi ushirikiano huo ambao ni wa kihistoria. Alisema Tanzania ijiandae na uwekezaji mkubwa kutoka kwa kampuni kubwa za Australia hususan katika masuala ya mafuta na gesi asilia.
Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava (katikati) katika picha ya pamoja na Balozi Geoff Tooth (wa pili kutoka kulia). Wa kwanza kushoto ni Afisa wa wizara ya Mambo ya Nje katika Idara ya Asia na Australia, Bertha Makilagi, anayemfuatia ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu Lusius Mwenda kutoka wizara ya Nishati na Madini.