Friday, November 28, 2014

WASICHANA WAHAMASISHWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI NA UFUNDI ARUSHA




WASICHANA WAHAMASISHWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI NA UFUNDI ARUSHA
Mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Arusha(ATC)Dk Richard Masika akizungumza kwenye tamasha la kuwahamasisha wasichana wanaosoma Shule za Sekondari kusoma masoma ya Sayansi na Ufundi inayofadhiliwa na serikali pamoja na serikali ya Ubalozi wa Italia. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji Safi na Maji Taka jiji la Arusha (Auwsa) akiwahamasisha wasichana kusoma masomo ya Sayansi na Ufundi hadi kufikia hatua za juu,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha ATC ,Dk Richard Masika na Mwakilishi wa Ubalozi wa Italia nchini,Daniel Christian.
Wanafunzi kutoka Shule za Sekondari 10 kwenye mikoa ya Arusha na Manyara wakifatilia tamasha hilo ambao waliahidi kusoma masomo ya ufundi ambayo yana uhakika wa ajira. 
 Mmoja wa wanafunzi kutoka Shule ya Arusha Sekondari aliyefanya vizuri kujibu maswali ya kisayansi akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi. 
 Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali.