USAJILI kwa watu wanaotaka kushiriki mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam umeanza rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent Melleck alisema, mara baada ya Dar es Salaam fomu za usajili zinatarajiwa kutolewa Dodoma kuanzia wiki ijayo.
"Tunapenda kutangaza rasmi kwamba usajili kwa ajili ya mbio hizo umeanza rasmi katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo kuna vituo zaidi ya 13 vilivyofunguliwa katika maeneo mbalimbali.
"Pia siku ya Jumanne na Jumatano wiki ijayo fomu hizo zitatolewa rasmi katika Viwanja vya Bunge, Dodoma ambapo Spika Anne Makinda ndiye anayetarajiwa kuongoza katika kujisajili.
Vituo vitakavyokuwa vikiuza fomu za ushiriki ni 1.Triple seven Mikocheni.2.maduka ya TSN,Uchumi supermarkets,Uwanja wa Leaderds Club,Ofisi za Rt Taifa,Standi kuu ya mabasi moshi mjini,Arusha na katika tovuti ya WWW.UHURUMARATHON.COM au kwa kupiga simu 0688108384
Mwaka huu pia kutakuwa na usajili wa vikundi mbalimbali na makampuni ambapo watashiriki kama vikundi ikiwa ni kuonyesha uzalendo wao.
Kwa taarifa hii napenda kuwaomba makampuni,mshirika binafsi na watu mbalimbali ambao wamekuwa wakiulizia kwa wingi kutaka kushiriki mbio za mwaka huu kuwa sasa wanaweza kuchukua fomu na kujaza na kurejesha mapema ili kuondoa usumbufu mkubwa unaoweza kujitokeza,Mwaka jana kulukuwa na msoongamano mkubwa sana sasa mwaka huu ni vyema tukachua fomu mapema ili kuepukana na usumbufu wa foleni kipindi cha mwisho alisema Melleck.
"Kingine mtu anayetaka kushiriki anaweza pia kujisali kwa njia ya mtandao wa internet na tunafanya utaratibu maalumu wa kuhakikisha pia yoyote anayetaka anaweza kujisaili kwa njia ya simu, "alisema.
Melleck alisema, katika usajili huo, fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 50,000 yule wa kilomita 5 Sh 5,000 na washiriki wa kilomita 21 watalipia Sh 10,000.
Mbio za mwaka huu pia zinatarajia kuhusisha shule za sekondari na msingi 25 ambazo zitashiriki katika mbio za kilometa 5
"Pia tunapenda kuchukua fursa hii kuziomba kampuni au taasisi mbalimbali zinazotaka kudhamini mbio hizo zijitokeze na kufanya hivyo, kwani nafasi bado ipo na tukumbuke bila amani hakuna chochote kinachoweza kuendelea, hivyo hata wao pia wanatakiwa kuipigania amani kwa nguvu zote."
Mbio hizo zinatarajiwa kushirikisha wanariadha kadhaa maarufu duniani.
Katibu wa Kamati ya maandalizi ya mbio za Uhuru wa Tanzania (Uhuru Marathon ),Innocent Melleck akionyesha fomu ya 3km ambayo itatumiwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete kwenye kushiriki mbio hizo na fomu hizo zinatarajiwa kuanza kuuzwa rasmi kesho katika vituo 13 jijini Dar Es Salaam na jumanne kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma ambapo spika Anna Makinda ataongoza wabunge kuchukua fomu za kuishiriki.
Katibu wa Kamati ya maandalizi ya mbio za Uhuru wa Tanzania (Uhuru Marathon ),Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari (hwapo pichani) jijini Dar Es Salaam juu ya maandalizi ya mbio hizo ambapo fomu za ushiriki zinatarajiwa kuanza kuuzwa rasmi kesho katika vituo 13 jijini Dar Es Salaam na jumanne kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma ambapo spika Anna Makinda ataongoza wabunge kuchukua fomu za kuishiriki.Kushoto ni mdau wa riadha,bwana Mroki Mroki.