Monday, November 10, 2014

Updates: JK aendelea vyema na matibabu anayopatiwa Marekani


Updates: JK aendelea vyema na matibabu anayopatiwa Marekani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini Marekani, leo Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume. 

Habari kutoka hospitalini hapo ambazo Globu ya Jamii imepata zinasema Rais Kikwete anaendelea vyema na leo asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo yote ni mswano. Tutaendelea kuwashirikisha kwa taarifa sahihi za  maendeleo yake mara kwa mara. Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani kulijenga Taifa.