Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema elimu imekomboa wanawake nchini Tanzania kwa kuwapa uwezo wa kushiriki sawa sawa na wanaume kwenye fursa za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe. Membe, ambaye alikuwa akihutubia kwenye mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Jijini Dar es Salaam leo, aliwataka wanawake kutumia kikamilifu fursa za elimu ya juu ili wajitegemee kiuchumi na kuondokana kabisa na unyanyasaji wa kijinsia.
Alielezea kuridhishwa na uwezo ulioonyeshwa na wahitimu wa kike katika chuo hicho. Kati ya wahitimu 902 waliotunukiwa Shahada na Stashahada na Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, 423 ni wanawake.
Mhe. Membe aliwataka wahitimu hao watumie elimu yao vizuri katika kuiendeleza jamii na taifa, kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
Brass Band ya Jeshi la Magereza ikiwaongoza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Kampasi ya Dar es Salaam , Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, Maafisa, Wahadhiri,Wahitimu pamoja na Wageni Waalikwa kuingia katika Viwanja vya Chuo Kikuu hicho katika sherehe za Mahafali ya Kumi na Moja ya chuo hicho yaliyofanyika tarehe 21.11.2014.
Mhe. Membe (mwenye joho la bluu) akiongozana na baadhi ya Wahadhiri kuingia katika viwanja yalikofanyika mahafali ya kumi na moja ya chuo kikuu cha Kimataifa cha Kampala Kampasi Dar es Salaam huko Gongo la Mboto.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi (mwenye kofia ya njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi Mhe. Membe (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama kwa heshima ya Wimbo wa Taifa kama ishara ya kuanza kwa mahafali hayo ya kumi na moja.
Shekhe Dr.Badruh H.Sseguja akifungua kwa sala Mahafali ya Kumi na Moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
Mchungaji Ogah Ogbole akifungua kwa sala mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Profesa Mohamed Ndaula akitoa hotuba ya ufunguzi wa mahafali hayo ya kumi na moja ya chuo hicho Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa fani mbalimbali wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Kampasi ya Dar es Salaam wakiwa wamekaa kwa utulivu tayari kabisa kwa ajili ya sherehe za mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho ambapo jumla ya wanafunzi 902 walihitimu masomo yao.
Baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala wakiingia katika viwanja vya chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam tayari kwa mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho.
Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja.
Mgeni rasmi, Mhe. Bernard Membe akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja ambapo aliwaasa kwenda kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala wakinyanyua kofia zao juu mara baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali yao ya kumi na moja ya chuo hicho.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria mahafali hayo wakifuatilia hatua kwa hatua kile kinachoendelea katika sherehe hizo.
Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala akitunuku shahada kwa wahitimu wa mahafali hayo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi ( mwenye joho la njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi, Mhe. Membe pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kwa heshima ya wimbo wa taifa kama ishara ya kufunga mahafali hayo ya kumi na moja.
Mgeni rasmi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahafali hayo. PICHA NA Reuben Mchome