Saturday, November 01, 2014

MDAHALO WA KUJADILI UMUHIMU WA KUZINGATIA MAMBO YA MSINGI KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UTAKAOFANYIKA KWENYE HOTELI YA BLUE PEARL, UBUNGO PLAZA DAR ES SALAAM JUMAPILI TAREHE 2 NOVEMBA 2014 KUANZIA SAA 9.00 MCHANA MPAKA SAA 12.00 JIONI



MDAHALO WA KUJADILI UMUHIMU WA KUZINGATIA MAMBO YA MSINGI KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UTAKAOFANYIKA KWENYE HOTELI YA BLUE PEARL, UBUNGO PLAZA DAR ES SALAAM JUMAPILI TAREHE 2 NOVEMBA 2014 KUANZIA SAA 9.00 MCHANA MPAKA SAA 12.00 JIONI
      Taasisi ya Mwalimu Nyerere inapenda kutoa taarifa kwamba imeandaa mdahalo wa Pili wenye lengo la kujadili umuhimu  wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba. Mambo ya msingi  yaliyomo katika Katiba hiyo yataainishwa  na kujadiliwa na washiriki wa Mdahalo.  Taasisi ya Mwalimu Nyerere inapenda kusisitiza kuwa lengo la mdahalo si malumbano au makatazo:

 Lengo ni kutoa fursa kwa washiriki wa mdahalo na wananchi kwa ujumla kujielimisha kuhusu Katiba inayopendekezwa ili waweze kuielewa vizuri, na hivyo kujiandaa kuipigia kura katika mazingira ya uelewa kwa kuzingatia dhamira yao, bila kulazimishwa, kutishiwa au hata kulipwa fedha na mtu au kundi lolote.  Hakuna kiingilio katika mdahalo huo, na watu wote wanakaribishwa.   

Mdahalo  utafanyika kati ya saa 9.00 mchana na saa 12.00 jioni  kwenye Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.  Washiriki wote wawe wamefika Blue Pearl  Hoteli  saa 8 mchana.

2.         Washiriki katika mdahalo huo ni baadhi ya waliokuwa Makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakiwamo  Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph S. Warioba,  Mzee Joseph W. Butiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bibi Mwantumu Malale, Mtumishi wa Umma Mwandamizi Mstaafu, ,   

 Ndugu Awadh Ali  Saidi, Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar na Ndugu Humphrey Polepole, Mdau wa Maendeleo),  Profesa Baregu, Jaji Mstaafu Mzee Ussi (Zanzibar) na Ndugu Muhammad Mshamba (Zanzibar).wananchi  na viongozi kutoka taasisi na asasi mbalimbali. zinazowakilisha jamii ya Watanzania ambazo ni pamoja na asasi za kiraia (NGOs), vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wasomi, vyombo vya habari, taasisi za kitaaluma, vyama vya ushirika vya wakulima na wafugaji, vyama vya wafanyakazi,  n.k. wanakaribishwa kushiriki.

3.         Mdahalo utarushwa moja kwa moja na ITV.  Kwa kupitia TV na Redio zao  na TV Sibuka Maisha.  Wananchi  po pote walipo wanaombwa kushiriki katika mdahalo huo.
Imetolewa na:

Mkurugezi Mtendaji,
Taasisi ya Mwalimu Nyerere,
S.L.P. 71000,
Fax No. 255 22 2119216/2118354
India/Makunganya/Bridge Street
1 Novemba,  2014