Friday, November 21, 2014

MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI AENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM


MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI AENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea ofisini kwake wakati akikabidhi Vifaa mbalimbali kwa wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini Ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi zake alizotoa Kipindi Akiomba kura ya Kuwa Mbunge wa Jimbo Hilo Pamoja za Ahadi anazotoa kwenye Mfululizo wa Ziara zake anazofanya Mara kwa mara katika Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood akikabidhi Mboa kwa Viongozi wa Msikiti kwajili ya Kumalizia ujenzi wa Msikiti ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa ziara zake za mara kwa mara.
 
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akikabidhi Tani 2O za Saruji kwa viongozi wa Kanisa la agae la Mjini Morogoro Kwajili ya kufanikisha Ujenzi wa Kanisa Hilo.
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akimkabidhi Tank la Maji Diwani wa kata ya Bigwa kwa niaba ya wakati wa kata hiyo Ili kutatua kereo ya Maji katiaka kata hiyo 
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akikabidhi Hundi ya Shilingi Laki Tano kwa kikundi cha wa mam wajasiriali Kutoka kata ya Kihonda  Magorofani
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikabidhi Hundi   
Katika Shuguli yake ya kukabidhi Vifaa mbalimbali Mh Abood alikabidhi vifaa vyenye Jumla ya Shilingi Milioni 1756OOOO/= Katika vikundi Mbalimbali vya Wajasiriamali,Vya Kidini kutoka kata za Jimbo la Morogoro Mjini.Baadhi ya Vifaa alivyokabidhi Mh Abood ni amoja na Matofali ,Vifyuko ya cement,Mabati Mbao na Hundi.
Akielezea zaidi Mh Abood alisema Maka sasa ameweza Kuchimba Visima  24 Kati ya 36 Vitakavyogharimu Kiasi cha Shilingi Milioni 365. Karibu  kata  Zote za Manisaa ya Morogoro Kwasasa Zina Kisima Kwajili ya kutatua changamaoto Kubwa ya maji inayowakumba wakazi wa Jimbo la Morogoro  Mjini.Akielezea zaidi Mh Abood Alisema Anapambana usiku na Mchana kutatua Kero Zote zinazowakumba wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini..
Akielezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na Ahadi zake alizotoa kwa wananchi wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Abood Amesema karibu ahadi zake zote alizoahidi Amezitekeleza ,Amewaomba wakati wa manisaa ya Morogoro Kushikiana nae Bega kwa Bega katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mainduzi.