Wednesday, November 05, 2014

Madereva watakiwa kutotumia simu wakati wanaendesha vyombo vya moto


Madereva watakiwa kutotumia simu wakati wanaendesha vyombo vya moto
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani nchini Kamanda Mohamed Mpinga,amewataka madereva nchini kuzingatia sheria za barabarani na kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.

Kamanda Mpiga, alitoa wito huo leo katika hafla ya kupokea pete maalum kutoka kampuni ya Vodacom ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayojulikana kama "Wait to Send" inayohamasisha madereva wa vyombo vya magari kuacha matumizi ya simu wanapokwa wanaendesha.

Pete hizo maalum ni za kuvaa kwenye kidole gumba ambapo madereva wanatakiwa kuzivaa wakiwa wanaendesha magari yao ili kuwakumbusha pindi wanapotaka kutumia simu

Alisema madereva wakizingatia sheria za barabarani  kwa kiasi kikubwa ajali zinazoendelea kutokea kila siku zitapunga na aliipongeza kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania na kampuni ya mafuta ya puma kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu.

Kwa upande wake,Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia alisema kampuni yao itaendelea kuunga mkono jitihada za kuondoa  matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu."Tunaomba madereva kufuata sheria za barabarani kwa usalama wenu na watumiaji wengine wa barabara.

Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu  ya mkononi  kupitia kampeni ya Wait to Send.Mbali na kampeni hii hii alisema kwa mwaka huu kampuni ilidhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.
Kamanda wa polisi wa usalama barabarani Mohamed Mpinga(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla maalumu ya kikabidhiwa stika na pete za kuvaa kwenye kidole gumba kwa madereva zenye ujumbe wa"wait to send" ukiwa na maana ya wateja wa simu za mkononi wasitumie simu zao za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo vya moto. kampeni hiyo imeanzishwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la usalama barabarani kupambana na janga la ajali barabarani.kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia na kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya mafuta ya puma Philippe Corsaletti.
Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kushoto)akimkabidhi stika Kamanda wa polisi wa usalama barabarani Mohamed Mpinga wakati wa hafla maalumu ya kikabidhiwa stika hizo na pete za kuvaa kwenye kidole gumba kwa madereva zenye ujumbe wa"wait to send" ukiwa na maana ya wateja wa simu za mkononi wasitumie simu zao za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo vya moto. kampeni hiyo imeanzishwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la usalama kupambana na janga la ajali barabarani nchini.
Kamanda wa polisi wa usalama barabarani Mohamed Mpinga,akionesha stika alizokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kushoto) wakati wa hafla maalumu ya kikabidhiwa stika na pete za kuvaa kwenye kidole gumba kwa madereva zenye ujumbe wa"wait to send" ukiwa na maana ya wateja wa simu za mkononi wasitumie simu zao za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo vya moto. kampeni hiyo imeanzishwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la usalama barabarani kupambana na janga la ajali barabarani nchini.
Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) na Kamanda wa polisi wa usalama barabarani Mohamed Mpinga wakionesha pete zenye ujumbe wa"wait to send" wakati wa hafla maalumu ya kikabidhiwa stika na pete hizo za kuvaa kwenye kidole gumba kwa madereva zenye ujumbe huo wenye maana ya wateja wa simu za mkononi wasitumie simu zao za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo vya moto. kampeni hiyo imeanzishwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la usalama kupambana na janga la ajali barabarani nchini.