Friday, November 21, 2014

KUMBUKUMBU



KUMBUKUMBU
Mama Mary John Mwingira
1946-2010

Leo Tarehe 21.11.2014 imetimia miaka minne (4) tangu utuache hapa Duniani Mama Mary Mwingira. Bado Kidonda ni kibishi mno.Maisha yetu sisi wanao, mama yako, wakwe , wajukuu, wadogo,wifi, wapwa, majirani, ndugu na marafiki zako wote yamebadilika na si kama ulivyokuwa nasi.

Tunakukumbuka na kuukosa upendo, ucheshi na uchapakazi na moyo wa kutokata tamaa uliokuwa nao. Umekuwa chachu ya maisha yetu na msaada mkubwa kwetu sote. Mungu alikuongoza kwa yote hadi kukujalia kifo chema ukiwa katika imani thabiti. Mapenzi yake MUNGU Baba yatimizwe kwani ndiye aliyetupa zawadi ya wewe kuwa mwanetu, mama yetu, bibi, dada, shangazi, mkwe, wifi shemeji, rafiki na jirani yetu mpendwa. Tunaahidi kuendelea kukuenzi daima kwa somo kuu lako la upendo usio na masharti.

Ulale salama mama yetu! Nasi tunakuombea kwa Mungu akupokee mbinguni ambako tunaamini umefika. Uendelee kutuombea sisi wanao na ndugu wote uliotuacha hapa duniani.Tunakupenda sana mama na kamwe hatutasahau mapenzi yako kwetu.

Machozi ni mengi machoni mwetu na hayapimiki kamwe. Tunashukuru kwa mafunzo ambayo yamezaa baraka na mafanikio tele. Ulikuwa hupendi kuona tunasononeka na tunaamini hadi sasa hupendi kutuona tukisoneneka hivyo tunasherehekea maisha yako matakatifu na tunasema, Asante MUNGU kwa zawadi hii kubwa ya kuwa watoto na ndugu zako..Umetuonyesha mfano wa kuigwa nasi wamama,wanawake na watu wengine wote mama Mwingira.

Tunakupenda na tuta kuenzi daima Milele na milele!!! Kutakuwa na Misa za kumuombea Mama Mary Mwinngira kanisa la Bethania, Tarehe 21 /11/2014- saa 12 unusu Asubuhi na vilaevile St Gasper Catholic Church –Kunduchi, Jumapili ya tr.23 Novemba 2014.

Misa hizi zitaendelea kwa mwezi wa 11 na 12 mwaka 2014 kila Jumapili St Gasper, Kunduchi misa ya 2(saa 1 kamili asubuhi).KARIBUNI SANA!!

Raha ya milele Umpe Eee Bwana,na Mwanga milele Umuangazie...Mary John Mwingira astarehe kwa AMANI..
AMEN