Na matukiodaimaBlogu. WAKATI maadhimisho ya siku ya mlipakodi nchini yameadhimisha leo nchini kote mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa imekabidhi tuzo mbili kwa a makampuni mawili yanayomilikiwa na familia ya kamanda wa UV CCM mkoa wa Iringa Bw Salim Asas likiwemo kampuni la usafirishaji mizigo la Asas Transporters Co. Ltd na ile ya usafilishaji wa mafuta ya TransFuel Logistics Ltd baada ya kuongoza kwa ulipaji mzuri wa kodi kwa mwaka 2013 /2014. Akitangaza washindi hao wakati wa maadhimisho ya siku ya mlipa kodi yaliyofanyika kimkoa katika ukumbi wa IDYDC mjini Iringa meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa Rosalia Mwenda alisema kuwa TRA imekuwa na utaratibu wa kuadhimisha siku ya mlipa kodi nchini na kuwa kwa mkoa wa Iringa na Njombe maadhimisho hayo yamefanyika katika mkoa wa Iringa kutokana na mamlaka hiyo kuendelea kufanya kazi kama mkoa mmoja . Alisema kuwa kampuni hizo za Asas zimeweza kuongoza katika ulipaji kodi katika kipengele cha mfanyabiashara mlipaji kodi mkubwa baada ya makampuni mawili yanayosimamiwa na Asas moja kushika nafasi ya kwanza ambalo ni lile kampuni ya usafirishaji ya Asas Transporters C. Ltd kwa ulipaji kodi na nafasi ya pili ya walipaji kodi wa kati pia imechukuliwa na kampuni ya usafirishaji mafuta ya Transfuel Logistics Ltd ambayo pia ni sehemu ya makampuni ya shiriki ya Asas Aliwataja wengine walioongoza katika ulipaji kodi kuwa ni pamoja na MT Huel Transporters , ambayo ilishika nafasi ya pili na nafasi ya tatu kwa walipaji kodi wakubwa ni pamoja na Ruaha University College huku upande wa walipaji kodi wa kati aliyeongoza na Iringa Foods and Deverages Ltd nafasi ya pili Transfuel Logistics Ltd na nafasi ya tatu Kalenga West Parki Tours MOtel Ltd . Wakati kwa wafanyabiashara wadogo walioshinda tuzo hizo za vyeti maalum nafasi ya ya kwanza alipewa BEder F. Kileo nafasi ya pili ilichukuliwa na Shakra Kiwanga ambae ni mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Ahmed Tasha wakati kwa mshindi wa jumla kwa mkoa wa Iringa na kanda ya nyanda za juu kusini akipewa tuzo hiyo Sao Hill Forest Project . Kwa upande wa vituo vya radio kampuni ya Big Time Hinghland co.Ltd(Radio Ebony Fm) nafasi ya pili kampuni ya Scope Tanzania Ltd ( Radio Countyr Fm) na nafasi ya tatu Qiblatain Fm Radio . Wakati kwa upande wa walipakodi bora wilayani kwa Mufindi ni SAo Hill Forest Project iliyoshika nafasi ya kwanza na ya pili na ya tatu kuchukuliwa na Chai Bora Ltd wakati wilaya ya Ludewa ni John Naoel Haule ,nafasi ya pili ni Donata Linus MGaya huku nafasi ya tatu ni Nathanael Mgaya , katika wilaya ya Makete aliyeongoza ni Felix Eliud Sanga , Christopher s. Mahenge na nafasi ya Tatu ni Shaibustolen Mahenge . Wilaya ya Njombe mshindi wa kwanza ni Philemon N . Mtewele nafasi ya pili ni Augustino L . Kisinga na nafasi ya tatu kwa ulipaji kodi ni Ndimi Enterprises Ltd . Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo mkurugenzi wa kampuni za Asas Bw Salim Abri asas ambae ni kamanda wa UV CCM mkoa wa Iringa alisem a kuwa wajibu wa kampuni yake ni kuendelea kulipa kodi vizuri kama sehemu ya kukuza uchumi wa Taifa na kuwa tuzo hizo ni heshima kwa kampuni zake na kuwa ni chachu kwa wengine kupenda kulipa kodi . Pia alisema wapo ambao wanafikra tofauti kuwa ukiwa mwanasiasa ni mtu wa kukwepa kodi na kuwa kampuni zake zipo kwa ajili ya kuona uchumi wa Taifa unakua pamoja na kulipa kodi kwa wakati na kwa mujibu wa taratibu za nchi . Hata hivyo alisema kuwa ukwepaji kodi hausaidii hata kidogo kwa ukuzaji wa uchumi wa Taifa na kuwa kila mfanyabiashara anapaswa kuwa mzalendo na Taifa lake kwa kulipa kodi badala ya kukwepa kulipa kodi . " Na mimi napenda kushukuru sana TRA kwa utaratibu huu wa kuwatambua walipaji kodi wazuri na kuwapa vyeti hii ni heshima na changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wengine kulipa kodi vizuri " |