Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Otilia Gowelle (kushoto) akizungumza jambo kuhusu msaada wa vifaa na vitabu vya miongozo kwa ajili ya mafunzo ya matabibu wasaidizi kwenda kwenye ngazi ya Tabibu viliovyokabidhiwa kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo na Elimu( I-TECH TZ), Dkt Fatma Kabore(kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
Mwakilishi Mkazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo na Elimu( I-TECH TZ), Dkt Fatma Kabore(kushoto) akimkabidhi tablet kwa ajili ya mafunzo ya masafa ya matabibu wasaidizi kwenda kwenye ngazi ya Tabibu Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Otilia Gowelle wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Kituo hicho kimekabidhi tablet 71 zenye thamani ya Sh. milioni 24 kati hizo 60 zitatumia na wanafunzi wa fani hizo kwenye vyuo vya Mtwara, Kilosa na Mafinga na nyingine zitatumiwa na wakufunzi.
Mwakilishi Mkazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo na Elimu( I-TECH TZ), Dkt Fatma Kabore(wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Otilia Gowelle(wa nne kutoka kulia) wakiwa na watendaji wengine wa wizara hiyo na kutoka kituo hicho.