Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youqing alipofika Wizarani tarehe 10 Novemba, 2014 kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao Mhe. Lu aliishukuru na kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa msimamo wake kuhusu tuhuma dhidi yake na China kuhusu biashara haramu ya pembe za ndovu na pia alisifu jitihada za Serikali ya Tanzania katika kupambana na biashara hiyo na kusema China inaunga mkono jitihada hizo na ipo bega kwa bega kuhakikisha inatokomezwa kabisa. |