Mkutano wa faragha wa Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa umeandaliwa na ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi ikishirikiana na UONGOZI Institute yenye lengo kuu ya viongozi hawa kujadiliana kuhusu mada kuu ya Mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmin, pamoja na maswala mbali mbali za kitaifa. Mkutano huu wa siku mbili ulifanyika tarehe 27-28 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
"Napenda kuishukuru sana Taasisi ya Uongozi, na Mtendaji wake Mkuu, Prof. Joseph Semboja, kwa mchango wao mkubwa katika kuandaa na kuendesha mikutano yetu hii, na juhudi nyingine za kujenga uwezo wa uongozi kwa watendaji waandamizi na wakuu ndani ya Utumishi wa Umma," alisema Balozi Sefue kwenye ufunguzi wa mkutano huu.
Mkutano ulikuwa na mada mbali mbali zinazohusu mifumo ya ufuatiliaji na tathmini, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa utekelezaji miradi ya kipaumbele, yaani Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now!) baada ya mwaka mmoja wa kutekeleza mfumo huo, pamoja na uzoefu kutoka Afrika Kusini kutoka kwa Dk. Sean Philips, Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kwenye Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini.
"Ukweli ni kuwa kila mahali duniani ambapo kumewekwa mifumo madhubuti ya ufuatiliaji na tathmini, iwe Serekalini au sekta binafsi, matokeo chanya na makubwa yamekuwa wazi na ya haraka," alisema Balozi Sefue.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifungua Mkutano wa faragha wa Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa tarehe 27 Oktoba, 2014.
Prof. Joseph Semboja, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi (UONGOZI Institute) akiratibu mkutano.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar, Dr. Abdullhamid Yahaya Mzee, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Tanzania, Balozi Ombeni Sefue na Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais – Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB), Bw. Omari Issa wakisikiliza mada.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria Mkutano wa faragha wa Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa mjini Dodoma leo Juma Tatu.
Dk. Sean Phillips, Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kwenye Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini, akitoa mada ya uzoefu wa Afrika Kusini katika ufuatiliaji na tathmini.