Thursday, October 16, 2014

Vikao vya Kamati za Bunge Oktoba na Novemba 2014



Vikao vya Kamati za Bunge Oktoba na Novemba 2014
Kamati ya Bunge ya Bajeti inatarajia kuanza vikao vyake kuanzia tarehe 13 Oktoba hadi 2 Novemba, 2014. Katika vikao hivyo Kamati inatarajia kushughulikia Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Tax Administration Bill, 2014) na Muswada wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (Value added Tax Bill, 2014). 
Katika kutekeleza azma hiyo, Kamati imepanga kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Tax Administration Bill, 2014) na Muswada wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (Value Added Tax Bill , 2014) siku ya Jumamosi hadi Jumanne ya tarehe 25 – 28 Oktoba, 2014 kuanzia saa 4:00 Asubuhi Ukumbi wa Mkwawa, Ofisi ya Bunge Dar es Salaam. Miswada hiyo itashughulikiwa kwa pamoja kutokana na maudhui yake kushabihiana. 
Kwa maelezo zaidi unaombwa kuwasiliana na Ndugu Michael Chikokoto simu Na.0785-570685 au Michael Kadebe kwa simu Na.0713-705463.


15 Oktoba 2014