Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kushoto) akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January MakambaOfisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kushoto) akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Ofisa Masoko wa Mauzo ya Jumla wa TTCL, Gipson Mosha akitoa maelezo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu ya huduma mpya ya uuzaji wa interneti 'IP Pop -Internet Protocol Point of Presence' iliyoanzishwa na kampuni hiyo.Ofisa Mratibu wa Ufundi wa TTCL, Mhandisi Anifa Chingumbe (kushoto) akitoa maelezo kwa baadhi ya wadau wa mawasiliano waliotembelea meza ya kampuni hiyo katika mkutano wa wadau wa mawasiliano wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mratibu wa Ufundi wa TTCL, Mhandisi Anifa Chingumbe (kushoto) akitoa maelezo kwa baadhi ya wadau wa mawasiliano waliotembelea meza ya kampuni hiyo katika mkutano wa wadau wa mawasiliano wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kushoto) akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wadau washiriki katika mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL wakifuatilia mkutano huo.
KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) imeanzisha kituo cha kuuzia huduma za interneti 'IP Pop -Internet Protocol Point of Presence' nchini ikiwa ni jitihada za kuboresha huduma za mawasiliano zaidi. Huduma kama hii awali ilikuwa ikinunuliwa nje hasa makampuni anuai yanayotoa huduma hizo barani ulaya.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota alipokuwa akizungumza na wanahabari katika mkutano wa wadau anuai wa mawasiliano kutoka nchi za Afrika Mashariki na baadhi za mataifa ya Afrika unaofanyika Tanzania. Ngota alisema kampuni ya TTCL imekuwa na mchango mkubwa wa kusimamia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwawezesha Watanzania na hata nchi jirani kupata mawasiliano mazuri kutoka katika nchi zao hadi katika nchi za ulaya.
"...Kuna juhudi mbalimbali TTCL tunafanya ili kuongeza fursa kwenye mawasiliano ambapo kwa sasa tumefungua kituo cha kuuzia interneti hapa nchini, kinaitwa IP Pop (Internet Protocol Point of Presence). Awali interneti tulikuwa tunaenda kununulia London kwenye makampuni mbalimbali sasa hivi tumeanzisha kituo chetu cha kununulia intaneti hapa hapa nchini...Kwa hiyo tunawakaribisha watumiaji wa interneti kuja kununua huduma hizi kwetu," alisema Ngota.
Akizungumzia mkutano huo, Ngota alisema wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo TTCL imejipanga vizuri kutumia fursa ambazo zinaweza kupatikana nchini na nje ya nchi ili kuendeleza sekta ya mawasiliano. "...Unapopiga simu lazima uende hadi nchi za nje kupata ile njia alafu ndo unarudi ulipo Afrika sasa hivi tunaangalia namna gani tutajikwamua na huduma kama hizo kuzipata hapa hapa Afrika..." alisema ofisa huyo wa TTCL.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akizungumzia mkutano huo alisema mkutano huo ni muhimu kwani wadau wa mawasiliano wamekutana kujadili maendeleo ya sekta ya mawasiliano, hasa katika ukanda wa afrika mashariki na afrika kwa ujumla. Alisema Tanzania inategemewa sana na nchi karibia saba ambazo zipo pembezoni mwa bahari kupitia huduma ya mkongo wake wa mawasiliano.
"Mkongo wa mawasiliano wa kimataifa umetua katika bahari yetu na sisi tunauza huduma hiyo kwa nchi nyingine...Tumeupeleka hadi kwenye mipaka ya majirani zetu kama Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na wengineo ambao hawana mawasiliano."
Makamba alisema mpango wa Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata mawasiliano mazuri na yalio bora maana hiyo ni haki yake. Sera na kanuni za Serikali ni kuhakikisha hilo linafanikiwa. Aliongeza kuwa kwa kulitambua hilo Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kujenga mkongo wa taifa wa mawasiliano.
"..Na sasa tunaingia kwenye awamu ya tatu ya upanuzi wa mkongo huo ikiwa ni sambamba na uboreshaji wa mawasiliano, ili ufike kila wilaya nchini, Watanzania wengi maeneo ya vijijini bado hawana mawasiliano, sehemu nyingine hakuna mawasiliano kabisa au pengine yapo lakini si mazuri.
Aidha alibainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2015 maeneo yote ambayo hayana mawasiliano yanapata mawasiliano, hii ni pamoja na kukaribisha makampuni mapya yaweze kuwekeza katika sekta hii ili uwepo ushindani kwamba kama kuna maeneo kampuni fulani haitaki kwenda basi nyingine ziende huko.
"...Mkongo wa taifa wa mawasiliano ni biashara na majirani zetu wanategemea na wananunua huduma hiyo kutoka kwetu. Tunachokifanya ni kuiimarisha kampuni ya TTCL hadi sasa wanafanya kazi nzuri sana wana wadau na washirika wengi toka nchi jirani ambapo wanafanya nao biashara. Kazi ya Serikali ni kuiwezesha ili biashara hiyo iwe kubwa zaidi," alisema Makamba.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com