Ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Wahitimisha Ziara yake Tanzania
Ujumbe wa wataalamu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ukiongozwa na Bw.Hervé Joly ulitembelea Tanzania kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 29 Oktoba 2014. Ujumbe wa IMF umefanya majadiliano ya tathmini ya kwanza ya Mpango wa Ushauri wa Sera za Uchumi (Policy Support Instrument -PSI) ulioidhinishwa na Bodi Tendaji ya IMF tarehe 16 Julai, 2014.
Ujumbe wa IMF ulikutana na Mhe. Mohamed Gharib Bilal , Makamu wa Rais wa Tanzania ,Mhe. Saada Mkuya Salum ,Waziri wa Fedha, Prof. Benno Ndulu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na maafisa waandamizi wa Serikali.
Ujumbe wa wataalamu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ukiongozwa na Bw.Hervé Joly ulitembelea Tanzania kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 29 Oktoba 2014. Ujumbe wa IMF umefanya majadiliano ya tathmini ya kwanza ya Mpango wa Ushauri wa Sera za Uchumi (Policy Support Instrument -PSI) ulioidhinishwa na Bodi Tendaji ya IMF tarehe 16 Julai, 2014.
Ujumbe wa IMF ulikutana na Mhe. Mohamed Gharib Bilal , Makamu wa Rais wa Tanzania ,Mhe. Saada Mkuya Salum ,Waziri wa Fedha, Prof. Benno Ndulu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na maafisa waandamizi wa Serikali.
Wakati wa kuhitimisha ziara, Bw. Joly alitoa taarifa ifuatayo:
"Matokeo ya kiuchumi kwa ujumla yameendana na matarajio chini ya Mpango wa PSI ijapokuwa changamoto mpya zimejitokeza katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita . Ukuaji wa uchumi uliimarika kwenye nusu ya kwanza ya mwaka 2014 na matarajio ni kukua kwa takriban asilimia 7 mwaka huu. Mfumuko wa bei umeongezeka kidogo miezi ya hivi karibuni hadi kufikia asilimia 6.6 mwezi Septemba kutoka na na bei kubwa za vyakula na mafuta. Aidha mfumuko wa bei kwa bidhaa zisizo za vyakula na nishati ulifikia kiwango cha chini katika historia cha asilimia 3.
"Malengo yote ya mpango wa PSI kwa mwaka ulioishia Juni 2014 yalifikiwa, isipokuwa lengo la ukusanyaji wa kodi. Licha ya kiwango kidogo cha ukusanyaji wa mapato katika mwaka wa fedha wa 2013/14 ikilinganishwa wa na matarajio ya bajeti,nakisi ya bajeti ilidhibitiwa na kufikia asilimia 4.4 ya pato la taifa ambayo ni chini ya lengo lililokuwa International Monetary Fund Washington, D.C. 20431 USA 2 limewekwa. Hata hivyo, kutokana na udhaifu uliopo katika uwezo wa kudhibiti matumizi, matokeo mazuri katika nakisi ya bajeti yaliendana na kuongezeka kwa malimbikizo ya madeni ya ndani. Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kuimarisha akiba ya fedha za kigeni hadi kuvuka lengo la mwishoni mwa mwezi Juni 2014.
Malengo ya mpango wa PSI kwa kipindi kilichobaki cha mwaka 2014/15 ,yanaweza kufikiwa ikiwa ni pamoja na lengo la nakisi ya bajeti lakini tahadhariza makusudi zinatakiwa katika kudhibiti matumizi ya serikali . Ukusanyaji wa mapato umeendelea kuwa chini ya lengo la bajeti katika robo ya kwanza ya mwaka.
Hata hivyo, fedha zote za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo zilitolewa baada ya Benki Kuu kuiwezesha serikali kubadili dhamana za serikali zilizotolewa kwa ajili ya kupunguza ujazi wa fedha na kuwa dhamana za serikali kwa ajili ya kugharamia bajeti hali hii ilileta changamoto katika utekelezaji wa sera ya fedha .
Vilevile , ucheleweshwaji wa fedha za wahisani wa maendeleo kutokana na suala la IPTL umeongeza changamoto katika utekelezaji wa mpango wa PSI .Hivyo basi ,wakati wa mapitio ya utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka ni vyema matumizi ya serikali ya kawianishwa na matarajio ya mapato. Utekelezaji wa mageuzi katika mfumo wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) mwanzoni mwa mwaka 2015 unatarajiwa kusaidia kuongezeka kwa mapato.
Ujumbe wa IMF umekubaliana na nia ya serikali kushughulikia kikamilifu malimbikizo ya madeni kwa wafanyabiashara na mifuko ya hifadhi ya jamii.
"Ujumbe umetambua hatua ya kwanza muhimu iliyochukuliwa katika kushughulikia suala la IPTL ambayo ni ukaguzi maaalum unaoendelea chini ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
"Majadiliano ya tathmini ya kwanza ya mpango wa PSI yamefikia hatua ya kuridhisha na yanatarajiwa kuhitimishwa wiki chache zijazo na baadaye kujadiliwa na Bodi Tendaji ya IMF mwanzoni mwa mwezi Januari 2015.
"Ujumbe wa wataalam wa IMF unatoa shukrani kwa majadiliano yenye tija na ya uwazi kwenye masuala ya kisera na kwa ukarimu wa dhati wa serikali wakati wa ziara.