Friday, October 31, 2014

Profesa Mwandosya atembelea mradi wa ujenzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia



Profesa Mwandosya atembelea mradi wa ujenzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia
Akiwa ziarani Ethiopia Waziri  wa Nchi (Kazi Maalum) Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya Mwandosya ametembelea mradi wa ujenzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia (Great Ethiopian Renaissance Dam-GERD).Ujenzi utakapokamilika mwaka 2017 GERD litazalisha MW 6000 za umeme na kuwa mradi mkubwa wa aina yake Afrika na wa nane kwa ukubwa duniani. Mradi unahusu ujenzi wa bwawa kwenye Mto Blue Nile, kilomita 850 kutoka Addis Ababa.
Waziri  wa Nchi (Kazi Maalum) Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya Mwandosya na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Naimi Aziz (wa pili kushoto) wakitembelea mradi wa ujenzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia (Great Ethiopian Renaissance Dam-GERD).
Waziri wa Maji Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Mheshimiwa Alemayehu Tegenu,kushoto,na Waziri wa Nchi (Kazi Maalum)Ofisi ya Rais,Mark Mwandosya ,kulia,wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi Mhandisi Bekele. 
Waziri Tegenu wa Ethiopia akiwa katikati mwenye kofia ya kijani,kulia kwake ni Mheshimiwa Naimi Aziz,Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, wa kwanza kushoto kwake ni Mama Lucy Mwandosya,mke wa Waziri Mwandosya, wa pili kushoto kwake ni Waziri Mwandosya,wa tatu kushoto kwake ni Mhandisi Bekele,Meneja wa Mradi,wakiwa na wahandisi wa mradi, na ujumbe wa Waziri Mwandosya. 
Eneo la Mradi wa ujenzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia (Great Ethiopian Renaissance Dam-GERD)