Thursday, October 02, 2014

NSSF YACHANGIA VIFAA VYA ICU HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI



NSSF YACHANGIA VIFAA VYA ICU HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Jumanne Mbepo (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 20 Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Marina Njelekela kwa ajili ya kununulia vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 
Kutoka kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Devota Ikandilo, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk John Kimario, Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Marina Njelekela na Ofisa Uhusiano wa NSSF, Jumanne Mbepo wakkwa katika picha ya pamoja baada ya NSSF kukabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 20 kwa ajili ya kununulia vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 
-----------------------------
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umechangia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Msaada huo utatumika kununulia vifaa kwa ajili ya chumba cha Wagonjwa mahututi (ICU).
 Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Dk. Marina Njelekela aliishukuru NSSF kwa msaada huo na kuongeza kuwa msaada huo utaenda kuokoa maisha ya watanzania wengi.
  Pia aliwashauri NSSF kushiriki kwenye clinic Maalumu ya upimaji wa Kansa ya Matiti kwa kina mama ambalo hufanyika hospitalini hapo.
Nae Mwakilishi wa NSSF, Jumanne Mbepo alisema kua mchango uliotolewa na NSSF kwa hospitali hiyo hautoshi kununua vifaa vyote na kuomba Taasisi nyingine ziichangie Hospitali hiyo ili kuweza kuokoa maisha ya Watanzania wengi zaidi.
NSSF imekuwa ikitoa huduma ya bima ya Afya kwa wanachama wake ijulikanayo kama SHIB , Hospitali ya muhimbili ni mojawapo ya watoa huduma wa bima hiyo.