Saturday, October 25, 2014

MTANDAO WA WANATAALUMA TANZANIA (TPN) WATOA ELIMU YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA


MTANDAO WA WANATAALUMA TANZANIA (TPN) WATOA ELIMU YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA
 Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile, akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Professional Approach Development, Lillian Madeje, akitoa mada kwenye kongamano hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
 Rais wa Mtandao huo, Phares Magesa, akihojiwa na wanahabari kuhusu ngongamano hilo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa Niaba ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal kwa ajili ya kufungua kongamano hilo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Mahmoud Mgimwa akihutubia katika kongamano hilo.
 Baadhi ya vijana wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
  Baadhi ya vijana wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
 Hapa mdau wa mtandao huo akijisali kwenye daftari la mahudhurio.
  Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Mahmoud Mgimwa (katikati), akiwa na viongozi wa mtandao huo. Kutoka kutoka kushoto, Naibu Katibu wa mtandao huo, Daniel Stephen, Rais wa Mtandao huo, Phares Magesa, Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile na Mjumbe wa Mtandao huo, Modesta Mahiga.
 Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo.

 Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali.
Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali.
………………………………………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale
 
WATANZANIA wametakiwa kujiunga katika fursa mbalimbali za kiuchumi ili kukuza maendeleo ya nchi katika kiwango kinachostahili.
 
Mwito huo umetolewa Dar es Salaam leo  na Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa kwa Niaba ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal wakati wa Ufunguzi wa wa kongamano la Mtandao wa Wanataaluma Tanzania(TPN).
 
Alisema kuwa ni wakati muafaka kujishughulisha na fursa za kiuchumi ili kufikia malengo ya millenia.
 
Alisema Serikali inaunga mkono jithada chanya zinazofanywa na sekta binafsi ambazo zipo kwa lengo la kuendeleza jamii na nchi kwa ujumla.
 
Mgimwa aliwata Watanzania wajiunge na TPN kwani una lengo la kuwahusisha katika sekta mbalimbali ikiwemo ujasiriamali ambao mara nyingi unakuwa katika kukuza maendeleo ya nchi.
 
"Watu wengi wanaweza kujiuliza kwamba wajiunge watapata nini lakini ukweli ni kwamba watanufaika na taaluma ambayo itakuja kuwasaidia katika maisha yao.
 
"Napenda niwapongeze kwani nimeona vijana wengi wamejiunga na mtandao huu ambao naamini utawasaidia vijana kuondokana na tatizo la ajira,"alisema.
 
Naye Rais wa TPN Phares Magesa alisema kuwa watu waache kusubiri kuwezeshwa badala yake wawe na mwamko wa kujiwezesha wenyewe.
 
Alisema lengo la sekta hiyo ni kutumia sekta ya ujasriamali katika kusaidia jitihada za Serikali  kukuza maendeleo ya nchini.
 
"Naamini kwamba kila kijana ambaye amehudhuria kongamano hili akitoka hapa anaweza kuwa mtu mzuri wa kujihusisha na ujasiriamali,"alisema.
 
Alisema kuwa maadhimio ya mkutano huo yatasaidia kutatua changamoto mbalimbali zionazpojitokeza katika jamii na kuweza kuzitatua kwa wakati.www. habari za jamii.com