Afisa Ushauri wa Vijana wa UNFPA – Tanzania Bi. Farida Juma malezo kuhusu njia sahihi ya matumizi ya Kondomu kwa baadhi ya vijana waliotembelea banda la UNFPA katika viwanja vya Maonyesh ya Wiki ya Vijana yanayofanyika mjini Tabora.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akigawa jarida la Si Mchezo kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Wizara hiyo katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana mjini Tabora.
Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Simon Peter akielezea kuhusu namna ya uandishi wa miswada ya Filamu kwa mmoja wa vijana awaliotembelea banda lao katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana mjini Tabora.
Afisa Vijana Mstaafu akitoa mada kuhusu Stadi za Maisha katika Kongamano la Vijana ikiwa ni kuadhimisha Wiki ya Vijana ambao Kitaifa inafanyikia mkoani Tabora.
Baadhi ya wadau wa Vijana wakifuatilia mada wakati wa Kongamano la Vijana kuhusu Stadi za Maisha lililofanyika mjini Tabora mapema hivi karibuni.
Vijana wa DSW wakifafanua kuhusu progamu ya Kijana Kwa Kijana inayoendeshwa na Shirika lao kwa kushirikisha vikundi vya vijana.
Baadhi ya Watumishi waWizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiangalia Vitabu wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana mjini Tabora.
Wadau wakiangalia Kahawa ya Ngara katika banda la Mkoa wa Kagera.
Mjasiriamali wa Mikoba na Batiki Bibi. Sophia Labani akimwelekeza mteja wake ubora wa bidhaa zake wakati wa Wiki ya Vijana inayofanyika kitaifa mjini Tabora. Picha Na Frank Shija, Tabora.