Na Editha Karlo wa Blog ya jamii
WIZARA ya Elimu na mafunzo ya ufundi imepigilia msumari wa kuendelea kuwazuia wanafunzi wa shule za sekondari na shule za msingi za bweni na kutwa kumiliki simu za mkononi wakiwa shuleni na yeyote atakayekamatwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Jenista Muhaga wakati wa mahafali ya kidato cha nne na darasa la saba wa shule ya sekondari ya Mwilayamvya medium iliyopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mkaguzi Mkuu wa shule kanda ya Magharibi Hadrian Mlelwa alisema kuwa serekali imeendelea kukazia mkazo wa kukataza suala la wanafunzi kuwa na simu mashuleni.
''ninachowaomba waalimu na walezi mashuleni wawe wanawasaidia wanafunzi pale wanapokuwa na matatizo kwa kutumia simu za shule au za ofisi kupiga kwa wazazi wao au walezi kueleza shida zao za si vinginevyo''alisema
Aliwataka wanafunzi hao kufuatilia masomo ambayo ndiyo yamewapeleka shuleni na wakimaliza masomo yao watakumbana na hayo mambo mtaani.
Naye Mkuu wa shule hiyo King Saguda alisema kuwa jumla ya wahitimu 219 walimaliza elimu ya msingi na sekondari huku wahitimu wa kidato cha nne 175 wakiwa ni na wahitimu wa darasa la saba wakiwa ni 24.
Mgeni rasmi katika mahafali ya saba kwa shule ya sekondari Mwilamvya Medium Hadrian Mlelwa kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu,Mh. Hadrian Mlelwa akisoma hotuba yake.
Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne ya darasa la saba shule ya sekondari Mwilamvya Medium Kasulu kwa Niaba ya waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Hadrian Mlelwa akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa shule hiyo kwenye chumba cha maabara pembeni ni Mkuu wa shule hiyo King Saguda.
Mkaguzi Mkuu wa shule kanda ya magharibi akisoma maelezo yalipo kwenye jiwe la mradi wa maji kaika shule ya Mwilamvya Medium baada ya kuuzindua mradi huo shuleni hapo.
Baadhi ya wahitimu wa darasa la saba katika shule ya Mwilamvya Medium Wilayani Kasulu wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi(ambaye hayupo pichani).
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwilamvya wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa hotuba yake.