Oktoba 14, mwaka jana Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa uliandaa hafla ya kwanza ya aina yake ya kumkumbuka na kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao hapa Umoja wa Mataifa na wageni mbalimbali. Ni hafla iliyoambatana na uzinduzi wa kitabu kinachomhusu Baba wa Taifa. Kitabu hicho kiliandikwa kwa ufundi mkubwa na Profesa Ali Mazrui kwa kushirikiana na Profesa Linda Mhando ambaye ni Mtanzania.
Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki Profesa Ali Mazrui. Ulitufunza mengi siku ile kumhusu Mwalimu na ambayo pengine hayajapatwa kuandikwa popote. Mwenyezi Mungu aiweke Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Profesa Ali Mazrui
Amen.