Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile, mchana wa leo ametiliana saini makubaliano ya mkataba wa kuanzisha Mradi wa Maji katika Wilaya ya Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro..
Dr. Likwelile alisaini Mkataba huo kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya uchumi ya Afrika. Aliye wakilisha Benki hiyo ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia.
Aidha katika kutiliana saini Mkataba huo Dr. Likwelile alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa Serikali ya Tanzania inatambua kuwa BADEA imetoa Dola za Kimarekani milioni 12.0 sawa na shilingi Bilioni 20.1 za Kitanzania kwa ajili ya kusaidia mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga.
Hivyo inatoa shukrani zake za dhati kwa BADEA kwa kusaidia kuchochea maendeleo ya Tanzania. "Msaada huu tulioupata leo utaisaidia Serikali kutatua tatizo la maji katika wilaya ya Same na Mwanga, hii inaonyesha ni jinsi BADEA unaunga mkono na kutekeleza jukumu zima la kushiriki katika masuala ya kijamii na ya kiuchumi kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo tunaomba muendelee kutusaidia". Alisema Dr. Likwelile.
Dr. Likwelile alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa, kama anavyofahamu gharama za mapendekezo ya mradi mzima ni Dola za Kimarekani million 110.43 na hii inahitaji uchangiaji kutoka katika mifuko mingine kama mfuko wa maendeleo wa Saudia , Mfuko wa Kimataifa wa OPEC na Serikali kuchangia fedha kusaidia mradi huu.
"Kwa hili sina wasiwasi nalo kwani ninafuraha kujua kwamba umeshakubaliana na ninaujasiri kuwa jitihada zako zitafanikiwa. Mradi huu wa maji wq wilaya ya Same na Mwanga unalenga kusaidia kuwepo kwa maji kwenye jamii mbalimbali zilizopo kwenye mradi huo." Aliongeza Dr.Likwelile. Aliendelea kusema kuwa,mradi huo utakapo kamilika:
(i) utaongeza kiwango cha watu wengi kuweza kupata maji safi na salama ya kunywa.
(ii) Uchumi wa Same na Mwanga utaimarika pamoja na hali ya afya kwa jamii nayo itakuwa imara hasa kwa maeneo yale yanayoguswa na mradi.
(iii) Hali ya maisha ya watu wa Same na Mwanga itainuka.
"Mafanikio ya ukamilishaji wa mradi huu ni muhimu sana kwa uchumi wa jamii na maisha bora kwa watu wa wilaya ya Same na Mwanga". Alisema Likwelile. Dr. Likwelilie alimalizia kwa kusema kuwa"Tanzania na Saudia ni marafiki wa muda mrefu sana, hivyo tutazidi kushirikiana na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa".
Imetolewa na: Ingiahedi Mduma
Msemaji - Wizara ya Fedha
Washington D.C
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akiwa na ujumbe kutoka Tanzania wakiwa tayari kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Aliye kushoto kwake ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia.Fedha hizo zimetoka BADEA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akitia saini makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Aliye kushoto kwake ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia. Aliyeko kulia ni Bi. Suzan Mkapa, Mkurugenzi wa sheria kutoka Wizara ya Fedha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakibadilishana mikataba hiyo baada ya kutiliana saini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakiionyesha mikataba hiyo kwa waliohudhuria sherehe hiyo baada ya kutiliana saini.