Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Mohd Dahoma, akifungua warsha ya kupitia sheria ya kudhibiti matumizi ya tumbaku Zanzibar iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resourt Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mshauri wa Ufundi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika William Onzivu akizungumza na washiriki wa warsha hiyo (hawapo pichani) katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resourt.
Afisa kutoka Bodi ya Mapato Tanzania (TRA) akitoa mchango katika warsha ya kupitia sheria ya matumizi ya tumbako iliyofanyika Hotelini hapo. Kulia Mwenyekiti wa warsha hiyo Dkt Mohd Dahoma.
Wajumbe wa warsha ya kupitia sheria ya kudhibiti matumizi ya tumbaku wakifuatilia sheria hiyo ilipowasilishwa na Mwanasheria wa Wizara ya Afya Amina Jabir (hayupo picha).(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).