Friday, September 26, 2014

Wiki ya nenda kwa Usalama ilivyoanza Kilimanjaro

Mwenyekiti wa Kamati ya usalama barabarani mkoani Kilimanjaro, Christopher Lyimo akimkabidhi zawadi mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa mkoa huo, Dk. Faisal Issa.
Kamanda wa Polisi wilaya ya Moshi, Hendry Mwakabonga, Mgeni Rasmi, Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Faisal Issa pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya usalama barabani, Christopher Lyimo, wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa.
Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Moshi, Hendry Nguvumali akisoma risala ya Kamati ya usalama barabarani kwa niaba ya Katibu wa Kamati hiyo, Kamanda wa usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro, Joseph Mwakabonga.
Sehemu ya maandamano katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani kimkoa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Stendi kuu ya Moshi.
Madereva wa Pikipiki za kusafirisha Abiria "Bodaboda" nao walishiriki maandamano ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani, ambayo kitaifa yalifanyika mkoani Arusha.
Dkt. Faisal Akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani.
Dkt. Faisal akikabidhi cheti cha ukaguzi kwa mmoja wa madereva ambao magari yao yalikidhio viwango vya ukaguzi.
Makamanda wa Jeshi la Polisi wa wilaya wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Moshi, Deudatus Kasindo (wa tatu kulia) pamoja na Meneja wa Tanroads Kilimanjaro, Marwa Rubrya (wa tatu kushoto) wakifuatilia kwa makini matukio uwanjani hapo.
Mgeni Rasmi akikagua Mabanda uwanjani hapo.Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii Kanda kaskazini.