Mkuu wa Kitengo cha Uragibishi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu Philomena Marijani akiwakaribisha walimu na wageni waalikwa wakati wa sherehe ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko katika Kijiji cha Nyamisati huko Wilayani Rufiji yaliyofanyika shuleni hapo tarehe 15.9,2014.
Baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungunzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu haokatika masuala ya jinsia na stadi za maisha. Hotuba hiyo ilikuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Elimu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Dkt. Mikidadi Alawi (hayupo pichani) tarehe 15.9.2014.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu katika Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Dkt. Mikidadi Alawi akifungua rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama. Waliokaa kushoto kwake ni Ndugu Obeth Mwakatobe, Makamu Mkuu wa Shule akifuatiwa ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo Ndugu Anitha Masaki kutoka Shirika la FAWE na Kulia kwa Mgeni rasmi ni Ndugu Philomena Marijani kutoka WAMA. Mafunzo hayo ya siku tano yalifunguliwa rasmi tarehe 15.9.2014 na yameandaliwa na Taasisi ya WAMA wakishirikiana na UNICEF.
Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama Ndugu Anitha Masaki kutoka Shirika la FAWE (Forum For African Women Educationalists-Tanzania Chapter) akitoa moja ya mada zake mara tu baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo shuleli hapo tarehe 15.9.2014.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo tarehe 15.9.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI.