Katibu wa Baraza kuu la Waisalam Mkoa wa Lindi (BAKWATA) Alhaj Abdillah Salum akifunga mafunzo kwa viongozi wa Kiislam pamoja na waalim wa madrasa katika Manispaa ya Lindi kuhusiana na Vita dhidi ya VVU/UKIMWI Chini ya Uwezeshaji wa AMREF kwa Ufadhili wa Global Fund.
viongozi wa dini ya kiislam wakipata mafunzo toka kwa mkufunzi wa mafunzo hayo,sheikh Shomari Mchongoma.
Maelezo ya Semina hiyo.
Na ABDULAZIZ ,Globu ya Jamii - Lindi
Viongozi wa dini mkoani Lindi wameaswa kuhimiza maadili mema kwa waumini wao ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili unaosababisha jamii kutenda matendo maovu ikiwemo kupiga vita ongezeko la maambukizi ya VVU na Ukimwi miongoni mwa jamii.
Wito huo ulitolewa na Katibu wa Baraza kuu la waislam (BAKWATA)Mkoa wa Lindi,Alhaj Abdillah Salum alipokuwa akifunga mafunzo ya elimu ya Kupambana na maambukizi ya VVU na UKIMWI kwa kwa waalim wa madrasa,Maimamu pamoja na viongozi wa Dini upande wa akina mama wa Manispaa ya Lindi.
Mafunzo Hayo ya jinsi ya kukabiliana na kuepuka maambukizi ya ukimwi kwa viongozi wa dini ya kiislam wa wilaya ya Lindi mjini yaliyofanyika mjini Lindi chini Usimamizi wa AMREF kwa Ufadhili wa Global Fund yameshirikisha jumla ya washiriki 50 na kuendeshwa na kitengo cha Ukimwi Bakwata Taifa(BAK-AIDS).
Alhaj Abdillah Salum alibainisha kuwa mafunzo hayo Yanatolewa kupitia Viongozi hao ili wasaidie kuirekebisha jamii kutoka kwenye mmomonyoko wa maadili unaosababisha itende maovu.
Masheikh zangu Kitengo cha ukimwi makao makuu kimeona ni vema kuwapa elimu hii kwa kuwa munayo nafasi kubwa kutokana na kuwa na wafuasi wengi mnaoweza kuwafikishia ujumbe kwa wakati kupitia maeneo ya Ibada na mafundisho ya Dini ili kuhakikisha VVU na Ukimwi inatokomea katika mkoa wetu....alimalizia Alhaj Salum.
Kwa upande wake mkufunzi wa masuala ya Ukimwi kitengo cha UKimwi,BAKWATA makao makuu,Shomari Mchongoma alisema mmomonyoko wa maadili unashamiri kutokana na wenye wajibu wa kuielimisha jamii kuacha kutimiza wao na kugeuka kuwa walalamikaji.
"Ongezeko la watoto wa mitaani ni matokeo ya wanaositahili kuielimisha jamii kupitia nafasi zao kukwepa jukumu hilo na kuishia kulalamika Hivyo viongozi wa dini tunalojukumu kubwa la kufikisha mahubiri kwa waumini wetu,ikiwamo namna ya kuepuka maambukizo ya Ukimwi hivyo jambo hili sio la kuiachia serikali peke yake"alisema Mchongoma.
Mafunzo hayo ya siku tatu ambayo yanafadhiliwa na AMREF yanalenga kuwajengea uwezo kwa viongozi hao wa dini ili kutambua mbinu za kukabiliana na maambu kizo ya UKIMWI yalifunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Lindi Dr Nassor Ally Hamid yakisimamiwa na Hamis Mayunga Afisa Tathmini Bakwata Makao Makuu.