Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati akizindua huduma ya LIPA KWA M PESA inayowawezesha wasambazaji wa huduma kupokea malipo ya mauzo kwa njia ya M-pesa kutoka kwa wauzaji wajumla. Kampuni ya Chai Bora na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia wasamabzaji wake kampuni ya Mahawi zimkuwa miongoni mwa wasambazaji wa awali kutumia huduma hiyo. Wengine pichani ni Mwakilishi wa Mahawi Enterprises Joseph Mahawi na kulia ni Meneja wa maendeleo ya Biashara wa Chai Bora Martin Ng'ethe.
aadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Chai Bora wakifuatilia mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa huduma mpya ya LIPA KWA M PESA inayowawezesha wasambazaji wa huduma kupokea malipo ya mauzo kwa njia ya M-pesa kutoka kwa wauzaji wajumla. Kampuni ya Chai Bora na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia wasamabzaji wake kampuni ya Mahawi zimkuwa miongoni mwa wasambazaji wa awali kutumia huduma hiyo.
Vodacom Tanzania imezindua huduma mpya ya M-PESA ijulikanayo kama "LIPA KWA M-PESA – huduma hii mpya ya kisasa ni jumuishi ya mfumo wa malipo utakao wezesha makampuni, mawakala wa jumla na rejareja na wafanyabiashara wengine kulipia bidhaa zao kwa kutumia M-PESA.
Huduma hii mpya imekuja ili kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na makampuni kwa kupanua mbinu za malipo kutoka kwa wafanyabiashara na makampuni na wauzaji wa aina mbalimbali, sasa mawakala wa jumla na rejareja wataweza kununua na kulipia bidhaaa zao kwa kutumia huduma hii ya LIPA KWA M-PESA. Njia hii mpya ni ya haraka, salama na inampa mteja wepesi zaidi wa kufanya biashara.
Akiongea kwenye uzinduzi huo,Bw. Kelvin Twissa , Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano alisemasema, "Vodacom imekuwa ikiongeza thamani na kusaidia kuboresha mbinu za ufanyaji wa biashara nchini kwa kuanzisha huduma ambazo zitaleta mapinduzi kwa jumuiya ya wafanyabiashara, ili kuepuka dhana za zamani za utendaji wa biashara. Huduma hii mpya ya LIPA KWA M-PESA ni ya haraka, salamaj, urahisi na na inamrahisihia mteja kuondokana na dhana ya kubeba hela nyingi kila saa ".
Wafanyabiashara wengi nchini wanapendelea kutumia fedha (cash) wanapo nunua na kuuza bidhaa zao, kwa sababu ni haraka. Hata hivyo nyakati hizi zinachangamoto kubwa ukifanya biashara kwa aina hiyo hasa wale ambao wanakipato kiasi na kikubwa cha fedha, aina hii ni tishio sana la kama wizi au hata pengine kuhatarisha maisha ya mfanyabiashara. Lakini sio ujambazi tuu hata pia ni gharama kubwa kusafirisha fedha na inagharimu muda mwingi wa wafanyabiashara.
Huduma hii mpya ya LIPA KWA M-PESA ni mapinduzi ya biashara, mfumo huu umeunganishwa kwanye akaunti ya mteja ya M-PESA na pia inaweza kuunganishwa na akaunti yako ya benki, ni kumuwezesha wafanyabiashara na wauzaji kulipia bidhaa mara moja, na shughuli zote hii zinafanyika kwa kupitia simu yako ya kiganjani. Mfumo huu mpya, unamuwezesha wakala aliejisajili kuweza kuweka hadi kiasi cha Tsh milioni 50 katika akauinti yake ya M-PESA tofauti na huduma ya M-PESA ya kawaida ambayo ina kikomo ya shilingi milioni 5. Mawakala wakubwa wanaweza kushikilia hadi Tsh bilioni 2 kwenye akaunti zao za M-Pesa. Hii ni fursa kubwa kwa jumuiya ya wafanyabiashara katika Tanzania kuanza kufanya biashara bila kua wanabeba noti kila saa.
Twissa anaendelea kusema "Huduma hii mpya ni rahisi, salama, na ya kuaminika na haina gharama yeyote. Sasa hivi mfanyabiashara haitaji tena kusafiri kwenda kutuma fedha, njia hii ni ya haraka zaidi; Unabonyeza simu yako tu marachache tu kuhitimisha biashara. Haihitaji makaratasi wala mtandao wa Internet kwani imeunganishwa moja kwa moja na mtandao Vodacom GSM."
Jinsi inavyofanya kazi ni rahisi sana, hakuna uwekezaji unao hitajika. Mara baada ya wakala kujisajili anaweza kufanya shughuli yake yote katika njia salama sana, mfumo unakupa taarifa ya mesegi (SMS) ya uthibitisho wa kila muamala unaofanya baina ya wakala na kampuni na unaemtumia pesa hizo na yeye anapata uthibitisho kua ni wewe unaemtumia wewe. Huduma yote hii ni bure na sasa hivi zaidi ya wakala 24,000 nchini kote tayari wamejiunga na huduma.
Akizungumza katika uzinduzi huo,Bw Olestus Mwalongo, ambae ni muuzaji wa vifaa vya ujenzi maeneo ya Buguruni, Dar es Salaam alisema "Nilitembelewa na Vodacom miezi sita iliyopita kwa kushiriki katika zoezi la kuitumia huduma hii, kabla ya kuletwa sokoni. Kwakweli faida ya huduma hii ni kubwa sana, kwanza utaratibu wake ni rahisi sana kama tu kama unapiga simu vile, pili unageuza maisha yako katika sura mpya. Zamani nilikua napata tabu sana kusafirisha fedha kwaajili ya kufanya malipo. Sasa hivi huduma hii imeniwezesha kupunguza gharama hizo na gharama zingine za uendeshaji. Sasa hivi nafanya biashara yangu kwa nafasi zaidi na nafarijika sana na huduma hii"
Kwa upande wake, Bw. Joseph Mahawi ya Mahawi Enterprises, wakala wa Serengeti Breweries alisema, 'Huduma hii ni salama na rahisi. Mimi sasa wanaweza kupokea malipo kutoka kwa wauzaji mbalimbali na kulipia mambo mengine huku nikipata taarifa za mahesabu yangu yote papo hapo. Huduma hii mpya inamfumo taarifa sahihi na ni kipengele kikubwa sana kwangu. Sasa naweza kusema biashara yangu inaenda vizuri sana na inaniruhusu mimi kufanya shughuli zingine. Sasa hivi nina muda zaidi wa kufikiria jinsi ya kukuza biashara yangu katika mwelekeo mpya. Zaidi ya hayo, siku hizi sipangi foleni kabisa kwenye taasisi yeyote ya fedha kusubiri kulipa wauzaji yangu. Sasa naweza kufanya hivyo nyumbani au mahali popote kwa furaha tu'.
Kujisajili na huduma ni rahisi; Wafanyabiashara na wauzaji unaweza kutembelea wakala yeyote wa Vodacom alie karibu yako kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujisajili. Vodacom imetenga dawati maalum la huduma kwa mteja wa LIPA KWA M-PESA.
Kwa maswali zaidi unaweza piga namaba 1500 muda wa wowote ndani ya masaa 24 siku zote za Juma bure.