Bunge La Afrika Mashariki Lilifikia Tamati Katika Vikao Vyake Vya Dar Es Salaam Kwa Kuahirishwa Kabla Ya Muda Wake Kutokana Na Akidi Kutotimia kufuatia Wabunge wa Burundi na Rwanda kutoka nje na Wengine Kutokuwepo.
Sheria Inataka Ili Kikao Kiendelee Lazima Bungeni Kuwe Na Nusu Ya Wabunge Wa Kuchaguliwa Na Angalau Wabunge Watatu Kutoka Kila Nchi Mwananchama.
Kikao Kiliahirishwa Baada Ya Rwanda Kuwa Na Mbunge Mmoja Na Burundi Wawili. Hii Ilikua Mara Ya Pili Baada Bunge Hilo Kuahirishwa Kwa sababu Kama Hizo Wiki Iliyopita.
Akizungumza Baada Ya Kuahirishwa Kwa Bunge Hilo Naibu Waziri Wa Afrika Mashariki Dkt Abdulla Juma Saadalla Alisema Serikali Imesikitishwa Na Vitendo Hivyo Vya Wabunge Kwakua Wanatumia Kodi Kubwa Ya Wananchi Wa Afrika Mashariki.
Bunge Hilo Lilianza Agosti 25 Na Lilitarajiwa Kuahirishwa Jioni Lakini Liliahirishwa Mchana.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki akiahirisha kikao cha Bunge hilo baada ya Akidi kutotimia kufuatia Wabunge wa Rwanda na Burundi kutoka nje na wengine kutokuwepo kabisa katika siku ya mwisho wa bunge hilo Ukumbi wa Karimjee Dar-es-Salaam Septemba 4, 2014.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Richard Sezibera akijibu hoja zilizoulizwa na Wabunge wakati wa kikao cha Bunge hilo Karimjee Dar-es-Salaam Septemba 4, 2014 kabla hakijaahirishwa kufuatia Wabunge wa Rwanda na Burundi kutotimiza akidi.
Naibu waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki Mh. Abdulla Juma Saadalla akijibu hoja wakati kikao cha Bunge la Afrika Mashariki Ukumbi wa Karimjee Dar-es-Salaam Septemba 4, 2014 kabla hakijaahirishwa.
Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea Bungeni katika Ukumbi wa Karimjee Dar-es-Salaam Septemba 4, 2014 kabla Bunge hilo kuahirishwa kutokana na Akidi kutotimua kufuatia Wabunge wa Rwanda na Burundi kutoka nje na wengine kutokuwepo kabisa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kikao cha Bunge la Afrika Mashariki Ukumbi wa Karimjee Dar-es-Salaam, Septemba 4, 2014.