Saturday, September 27, 2014

Vijana wahamasishwa kutembelea vituo vya afya kujua afya zao


Vijana wahamasishwa kutembelea vituo vya afya kujua afya zao
Msanii wa Muziki wa Taarabu na mpiga Gitaa maarufu nchini Bw. Thabit Abdul akizungumza na vijana wa jijini la Dar es Salaam wakati wa hafla ya Jamvi la Vijana ambalo uendeshwa maramoja kila mwezi na Kituo cha Vijana UMATI kilichopo wilayani Temeke alipokuwa mgeni rasmi katika jamvi hilo jana jijini Dar es Salaam. Jamvi hilo lilikuwa na ujumbe mahususi kwa vijana uliolenga kuwa hamasisha kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kupata matibabu.
Mratibu wa Kituo cha Vijana cha UMATI kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam Bi. Upendo Daud akifafanua jambo kwa vijana waliohudhuria Jamvi la Vijana katika kituo hicho jana jijini Dar es Salaam. Ambapo jamvi hilo lilikuwa na ujumbe mahususi kwa vijana uliolenga kuwahamasisha kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kupata matibabu.
Msanii wa Muziki wa Taarabu na mpiga Gitaa maarufu nchini Bw. Thabit Abdul akipima kwa hiari Virusi vya Ukimwi jana jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuhamasisha vijana kujitokeza kujua afya za na kupata matibabutukio hilo limefanyika jana alipokuwa mgeni rasmi katika ya Jamvi la Vijana ambalo uendeshwa mara moja kila mwezi na Kituo cha Vijana cha UMATI kilichopo wilayani Temeke. Jamvi hilo lilikuwa na ujumbe mahususi kwa vijana uliolenga kuwa hamasisha kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kupata matibabu.Kushoto ni Mnasihi wa Kituo hicho Bibi. Neema Orgeness.
Msanii wa Muziki wa Taarabu na mpiga Gitaa maarufu nchini Bw. Thabit Abdul akipata maelekezo ya matumizi sahihi ya Kondomu kutoka kwa mueleisha Rika wa Kituo cha Vijana cha UMATI kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam Bi. Mwanahamis Issa(kushoto) alipo kuwa mgeni rasmi katika Jamvi la Vijana ambalo ufanyika kila mwisho wa mwezi.Mwezi huu jamvi hilo lilikuwa na ujumbe mahususi uliolenga kuwa hamasisha vijana kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kupata matibabu.Kushoto ni Mnasihi wa Kituo hicho Bibi. Neema Orgeness.
Kikundi cha Sanaa cha Malezi kikitoa burudani kwa vijana wakati wa Jamvi la Vijana jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa Jamvi la Vijana wakifurahi burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali waliotumbuiza na kutoa burudani katika Jamvi la Vijana lilofanyika jana jijini Da es Salaam. Jamvi la Vijana uendeshwa mara moja kila mwezi na Kituo cha Vijana cha UMATI kilichopo wilayani Temeke kwa mwezi huu Jamvi hilo lilikuwa na ujumbe mahususi kwa uliolenga kuwahamasisha vijana kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kupata matibabu. PICHA NA FRANK SHIJA, MAELEZO