Thursday, September 18, 2014

Uongozi wa kampuni ya Nyumba ya NAKHEEL, ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai watembelea NHC, wafanya Mazungumzo



Uongozi wa kampuni ya Nyumba ya NAKHEEL, ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai watembelea NHC, wafanya Mazungumzo
Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga (kulia) akiongozana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai ambayo ni wawekezaji wakubwa duniani katika sekta ya uendelezaji miliki, Rashid Ahmed Lootah, kuingia kwenye chumba cha mikutano cha Ofisi za 

Mkurugenzi Mkuu wa NHC jiji Dar es Salaam jana, nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ujenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo, Masood Al Zarooni na Injinia Fawzi Al Shah ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mipango Miji wa Kampuni hiyo.

Mwenyekiti huyo na ujumbe wake wakiongozwa na Balozi Mjenga walikuwa na mazungumzo na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa kuhusiana na fursa za uwekezaji zilizopo katika Satellite Cities na Fursa za Kujenga uwezo wa masuala mbalimbali katika uendelezaji miliki.  

Baadhi ya miradi iliyosimamiwa na kampuni hiyo ni pamoja na The Palm Dubai (the largest island Palm City in the World), Nakheel Mall, Dragon Mart na baadhi ya hotel za nyota tano Jijini Dubai.