Thursday, September 18, 2014

Tanzania yashiriki maonesho ya 7 ya masuala ya Petroli na Mafuta nchini china

Wadau wa Mafuta na Gesi kutoka nchini Tanzania wakisikiliza kwa makini maelezo ya teknolojia mpya za utafiti wa mafuta na gesi Duniani huko nchini China. Wadau hawa walihudhuria maonesho ya 7 ya kimataifa ya mafuta, gesi na bidhaa zitokanazo na rasilimali hizo yaliyofanyika katika jiji la Dongying nchini China. Maonesho kama haya hufanyika kila mwaka yakilenga kujenga uhusiano baina ya nchi nan chi na pia kubadilishana uzoefu katika sekta ndogo ya mafuta na gesi duniani.
Bw. Ibrahim Rutta, mdau kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) akipata maelezo juu ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kutoka kwa mmoja wa wanamaonesho huko nchini China. Hiyo picha hapo chini inaonesha mfano wa kiwanda cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kama kile kinachojengwa na Tanesco na kusambaziwa gesi asilia na TPDC pale kinyerezi.