Monday, September 15, 2014

TAARIFA YA KAMISHNA KOVA KWA WANANCHI


TAARIFA YA KAMISHNA KOVA KWA WANANCHI
Kamishina Kova akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani).


Baadhi ya vitu mbalimbali vilivyokamatwa na jeshi la polisi.
 KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Suleiman Kova leo, ametoa taarifa maalum ya Jeshi la Polisi kuhusiana na mafanikio  katika utendaji wao wa kazi.
Kova ametoa taarifa  ya matukio yaliyojitokeza katika kipindi cha wiki mbili ikiwemo operesheni maalum ya kuzuia kupambana na matishio ya uhalifu jijini Dar es Salaam, mtandao wa uhalifu wanaotumia teknolojia ya mawasiliano (IT).

Kukamatwa kwa majambazi sugu wawili pamoja na SMG, kukamatwa kwa tiketi bandia 424 za mechi ya ngao ya hisani kati ya Yanga na Azam pamoja na  Kupatikana kwa silaha aina ya Pistol na risasi 6.