Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt,Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya muendelezo wa harakati zake za kusaidia kuimarisha ulinzi wa Wanyama aina ya Tembo ili wasiuwawe hapa nchini,ikiwa ni Bia iliyobeba jina la Mnyama huyo,ambapo wametoa vifaa mbali mbali vya kusaidia ulinzi huo,ikiwa ni pamoja na Darubini kubwa (Binoculars) na trimble GPS ambazo zitasaidia katika harakati za kupambana na ujangili katika mbuga za wanyama nchini.Kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari kwenye Mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa TBL jijini Dar es Salaam,ikiwa ni pamoja na upokeaji wa vifaa kutoka kwa bia ya Ndovu Special Malt.Kulia ni Meneja wa Bia ya Ndovu,Pamela Kikuli
Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika hifadhi ya Serengeti,Agricola Lihiru akielezea namna ya matumizi ya vifaa hivyo na faida yake katika kupambana na ujangili kwenye hifadhi za wanyama nchini.
Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt,Pamela Kikuli akikabidhi baadhi ya vifaa hivyo kwa Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete na Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika hifadhi ya Serengeti,Agricola Lihiru.Picha zote na Othman Michuzi.