Friday, September 19, 2014

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AKUTANA NA WAENDESHA PIKIPIKI SONGEA


MKUU WA MKOA WA RUVUMA AKUTANA NA WAENDESHA PIKIPIKI SONGEA
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akizungumza na waendesha pikipiki (Maarufu kama  Boda Boda) leo hii katika ukumbi wa Songea Club uliopo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma. Mwambungu amewataka dereva Boda boda kuepusha ajali za barabarani kwa kufuata sheria,kutotumiwa katika maandamano ya kisiasa ambayo yanapelekea uvunjifu wa amani na kuwafanya wapoteze maisha ama kuwafanya kuwa walemavu.
 Pichani ni umati wa waendesha pikipiki wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakimsikiliza mkuu wa Mkoa  ambaye hayupo pichani. Ambapo katika mkutano huu amewaasa mambo mengi ikiwemo suala lililotokea hivi karibuni la kuwarushia bomu askari polisi waliokuwa kwenye doria na kuwajeruhi askari wa tatu.
Madereva pikipiki hawa wakimsikiliza mkuu wa mkoa kwa umakini huku wakiahidi kutoa ushirikiano wa kuwafichua wahalifu ambao wamejiingiza katika huduma ya kusafirisha abiria kwa lengo la kuwachafua na wao kukidhi mahitaji yao.
Piki piki zikiwa zimepaki nje ya mkutano.(Picha zote na demasho.com)