Tuesday, September 23, 2014

Mkuu wa Mkoa wa Arusha aikabidhi ngao Vodacom Tanzania kwa kutambua mchango wake kuhakikisha usalama barabarani



Mkuu wa Mkoa wa Arusha aikabidhi ngao Vodacom Tanzania kwa kutambua mchango wake kuhakikisha usalama barabarani
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw.Magessa mulongo, akimkabidhi ngao Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa kwa kutambua mchango na jitihada za Vodacom kuhakikisha usalama barabarani,ngao hiyo ilikabidhiwa wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani yamefanyika kitaifa mkoani Arusha,kampuni ya Vodacom ni moja wa wadhamini wakubwa wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwaka huu
Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa akiwa na maofisa wa jeshi la polisi wakisilikiza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Bw.Magessa mlongo,wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani ambayo imefanyika kitaifa mkoani Arusha,ambapo Vodacom Tanzania wamepewa tunzo ya kutambulika kwao katika kutoa mchango na jitihada za kuhakikisha usalama barabarani,Tuzo hiyo wamekabidhiwa katika siku ya ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwaka huu.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani wakimuangalia mtaalamu wa masuala ya uokoaji Bw. Nelson Gachiru,aliyekuwa kwenye moja ya banda la maonyesho katika uwanja waSheikh Amri mjini Arusha,Vodacom Tanzania ni moja ya wadhamini wakuu wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwaka huu na kuweza kujinyakulia ngao ya kutambulika kwa mchango wake na jitihada za kuhakikisha usalama barabarani.