Mama Fortunata Joseph Msoka. Hatimaye leo umetimiza mwaka mmoja tangu ulipotuacha Watoto wako, Wadogo zako, Shemeji, Wifi, Wajukuu zako, Wakwe zako, Wanajumuia wenzako na majirani zako kwa majonzi makubwa yasiyoelezeka.
Lakini Tunaamini kwamba yote ni mapenzi ya Mungu aliyekupenda zaidi. Ibada ya kumwombea itafanyika Jumapili 21/09/2014 Kanisa Katoliki la Mt. Augustino Ukonga saa 2:30 Asubuhi.
Kwa hakika pengo lako halizibiki. Unakumbukwa na watoto wako wapendwa Paul Msoka, Rose Mdami, Constantine Msoka, Jackline Msoka,Wajukuu zako, kaka zako, wadogo zako, shemeji zako, wifi zako, wakwe wako, WAWATA Ukonga, Jumuia yako na Parokia yako penzi ya Mt. Augustino Ukonga.
Tunafarijika sana na Zaburi ya 147 na Zab 148 inayotutaka kumsifu, kumwabudu, na Kumshukuru Mungu daima kwa ajili yako. "Mungu akulaze mahali pema mbinguni, Upumzike kwa Amani. Amina"