Monday, September 22, 2014

KINANA ASISITIZA WANANCHI BAGAMOYO KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA YA JAMII



KINANA ASISITIZA WANANCHI BAGAMOYO KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA YA JAMII
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwapungia mkono wakazi wa Bagamoyo wakati wakiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa shule ya Msingi Jitegemee.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi mshahiri maarufu wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Ali Pongwe baada ya kutoa ushairi mzuri kabla ya kuanza kwa mkutano.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo ambapo aliwasisitiza kujiunga na mfuko wa afya ya jamii pamoja na wazazi kuwapeleka watoto shule pia aliwashauri wazazi kuchagua watu wenye shughuli zao kuingia kwenye kamati za shule kwani kutasaidia sana kupunguza michango isiyo ya lazima.
 Wananchi wa kata ya Magomeni wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni na kuwataka kuhakikisha watoto watakaochaguliwa kuingia sekondari wanaenda shule kwani kushindwa kufanya hivyo ni kurudisha nyuma maendeleo.Pia aliwataka wananchi wachunge afya zao kwani elimu ya maambukizi ya ukimwi inatolewa ya kutosha hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na afya yake.
 Sehemu ya watu waliohudhuria mkutano.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni ambapo alitoa sifa kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani kwa utendaji wake wenye ufanisi mkubwa pia aliwaambia wananchi hao kuwa vyama vya siasa ndio vimeshafika muda wake kwani havina sera na vimeshindwa kuja na sera mbadala ya kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini.
 Wananchi wakimsikiliza Nape Nnauye ambaye pia aliwataka watendaji wa Serikali kuwa karibu na wananchi kwani kutasaidia kufanikisha maendeleo na kuondoa sintofahamu za wananchi wanaotaka kujua taarifa za maendeleo ya miradi au maeneo husika.
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk.Shukuru Kawambwa akihutubia wakazi wa jimbo lake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Jitegemee ambapo aliwaambia kero za michango midogo midogo zinaondolewa .
 Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni ambapo aliwaambia  wanawake kutokuwa nyuma katika kuomba nafasi za uongozi katika chaguzi zinazokuja.
 Mmoja wa wananchi waliofika kwenye mkutano akiuliza swali kwa Katibu Mkuu wa CCM wakati wa mkutano .

 Diwani wa kata ya Magomeni Bi.Mwanaharusi Jarufu akijibu moja ya maswali yaliotoka kwa wananchi.
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo akijibu maswali kutoka kwa wananchi
Sehemu ya wanachama wapya waliopokea kadi zao za uanachama leo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo zaidi ya wanachama 338 walijiunga na CCM.(Picha na Adam Mzee)