Tuesday, September 16, 2014

KAMPENI YA MWANAMKE NA UCHUMI SASA KUHAMIA TANGA



KAMPENI YA MWANAMKE NA UCHUMI SASA KUHAMIA TANGA
 Mkurugenzi wa Angels Moments inayoendesha Kampeni ya Mwanamke na Uchumi, Naima Malima akitoa hotuba ya ufunguzi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani mwanza hivi karibuni. Kampeni hiyo yenye lengo la kuwawezesha kiuchumi wanawake wajasiriamali ambapo kampeni hiyo itafanyika mkoani Tanga Mwezi Oktoba. Picha na Angels Moments.
 Mshairi maarufu bibi sauda akitoa burudani ya mashairi yake adhimu kwa lugha ya kufurahisha na burudani kwa wanawake wajasiliamali katika kampeni ya mwanamke na uchumi jijini mwanza.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilemela ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kampeni ya Mwanamke na Uchumi iliyofanyika Mwanza, Mh. Halima Masenza akifurahia mashairi ya Bi. Sauda (hayupo pichani) katika kughani mashairi yake kwa lugha ya kiswahili.