Likirudi kwa mwaka wake wa saba, tamasha la magari Tanzania (autofest) litakua likionyesha magari mapya, matoleo mapya ya pikipiki, burudani za muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wa nchini na burudani nyingine za kusisimua kwa ajili ya familia nzima kuanzia Septemba 19-21, 2014. Tamasha la mwaka huu ambalo linaandaliwa na Vision Investment, litafanyika katika viwanja vya Biafra, Kinondoni. Anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi ni Mhe. Dk Abdallah O. Kigoda, Waziri wa viwanda na Biashara.
''Tukio hili linahusisha moja ya maonyesho muhimu sana na yenye mvuto katika ulimwengu wa vyombo vya moto". Alisema Ally Nchahaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investments. "Lengo letu ni kuendelea kuleta aina mbalimbali ya bidhaa ya vyombo vya moto na huduma kwenye 'Autofest' ili wadau wapate kufurahia na kuridhishwa navyo." alisema.
Tukio hili la mwisho wa wiki linategemea kuvutia zaidi ya watu nusu milioni, na kulifanya kuwa tamasha kubwa na maarufu la magari Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008, Autofest sasa imekua ni Tamasha muhimu katika ulimwengu wa vyombo vya moto, likiwa ni onyesho pekee linalowaleta wapenzi wa magari pamoja. Ni onyesho kubwa linaloonesha magari ya abiria, magari ya biashara, pikipiki, bodi za magari, sehemu za magari, mashine na zana zinazohusiana na magari.
Burudani kwenye tukio zitahusisha, 'Bumper to Bumper Auto Style Zone' ambayo ni nafasi kwa wapenzi wa magari kuonyesha walivyoyapamba magari yao, 'Kids Car Zone,' ambayo itawaburudisha watoto wa umri kati ya miaka mitano na 14 kwa program za magari na elimu muhimu ya magari na usalama barabarani, na kuweza kuburudika na mbinu mbalimbali za kuchezesha magari kama kubadilisha gia, "Mwaka huu tunatarajia kwamba matokeo yatakua makubwa zaidi ukilinganisha na mwaka uliopita kutokana na kuongezeka kwa matangazo na mahusiano ya umma," alisema Nchahaga. "Autofest itapelekea kutambulika kwa wadhamini wetu na program." alisema.
Tamasha la Autofest linatoa nafasi za udhamini na maonesho. Kampuni ya Vision Investment inakaribisha wadhamini na watu wanaotaka kushiriki katika maonyesho ya mwaka huu kwa kujaza fomu ya maombi iliyopo katika mtandao wa www.autofest.co.tz. Fulana za Autofest sasa zinapatikana kwa mauzo, na mapato yatayopatikana yatatumika katika kuendeleza program za Autofest.