Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya kimataifa ya vijana duniani kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kushoto ni Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga na kulia ni Mtaalamu wa Programu za Vijana kutoka UNFPA, Tausi Hassan.
.Siku ya vijana duniani na ujumbe wa "Vijana na Afya ya Akili"
.Takwimu zinaonyesha nusu ya idadi ya watu nchini ni vijana
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI Kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imeahidi kukuza na kuboresha misingi ya kuwashirikisha vijana katika utekelezaji wa sera mbalimbali, programu na mikakati ya maendeleo.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Sihaba Nkinga, wakati wa maadhimisho ya siku ya vijana duniani kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam, Bibi Venerose Mtenga amesema kwamba lengo la kuwashirikisha vijan ni kuhakikisha kuwa sauti zao zinasikika na kufanyiwa kazi.
"Katika kutekeleza eneo hili Tanzania inalenga kuweka fursa zitakazowawezesha vijana kukuza utaalamu na ujuzi utakaowawezesha kufanikiwa katika kipindi cha mpito kutoka ujana kwenda katika utu mzima," amesema Bibi Mtenga.
Amesema kwamba Tanzania kama sehemu ya dunia inatambua changamoto maalum zinazowakabili vijana walioko katika mazingira hatarishi pamoja na umuhimu wa kuhakikisha kuwa vijana wanahusishwa kikamilifu katika malengo ya maendeleo
Timu ya wasichana ya mpira wa kikapu ya Don Bosco Lioness kwenye picha ya pamoja na Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga.
Timu ya waichana ya Don Bosco Lioness wakijipiga u-selfie baada ya kuibuka kidedea kwenye maadhimisho hayo.