Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na wanafunzi wa Makete Girls Sekondari (hawapo Pichani) na pia kutoa maagizo kwa uongozi wa shule.
Shule ya sekondari ya wasichana (Makete Girl's) imetii agizo la mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro la kutaka wanafunzi hao wapewe uji mara baada ya vipindi viwili vya asubuhi badala ya saa nne agizo alilolitoa Agosti 8 mwaka huu
Hali kadhalika mkuu huyo aliagiza wapewe chakula cha mchana saa saba ili kuweka uwiano mzuri wa muda wanaokula wanafunzi hao wawapo shuleni hapo
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Mwandishi wetu aliyefika shuleni hapo ijumaa ya Agosti 22, ameshuhudia maagizo hayo yakitekelezwa jambo ambalo limepongezwa kwa kiasi kikubwa na wanafunzi hao
"Ni kweli tumeshuhudia ratiba ya chakula ikibadilika kama alivyoagiza mkuu wa wilaya aliyokuja hapa shuleni, na kweli tunaona ni afadhali na tutajisomea vizuri na limetekelezwa mara tu alivyoagiza hivyo naupongeza uongozi wa shule kwa kutekeleza hilo" alisikika akisema mwanafunzi mmoja
Katika hatua nyingine shirika la sumasesu limetoa elimu ya ujinsia kwa wanafunzi hao na kuwataka kujiepusha na vitendo vya ngono ilihali wao ni wanafunzi ili waweze kufikia malengo yao
Rai hiyo imetolewa na Bi Anifa Mwakitalima na kusema kuwa wao ni wanafunzi wa kwanza katika shule hiyo na wanategemewa kufaulu na kuweka sifa nzuri kwa wilaya, hivyo itakuwa nia aibu kubwa kwa mwanafunzi kuweka historia ya kuwa mwanafunzi wa kwanza kusoma katika shule hiyo na pia akawa wa kwanza kupata mimba na kufukuzwa shule
"Ninani anayependa awe wa kwanza kupata mimba na kuandika historia mbaya kwa shule? bila shaka hakuna, wadogo zangu nawaomba mzingatie masomo achaneni na ngono kabisa muda wenu bado, huu ni muda wa kusoma" alisema Mwakitalima
Kwa upande wake Faustine Mwenda amewataka wanafunzi hao kujitambua kuwa wamepelekwa shuleni kwa ajili ya kusoma hivyo wajisomee na watafaulu vizuri hivyo kujijenge amsingi mzuri wa maisha pasipo kupata shida
Amesema mafanikio yao yanajengwa na wao wenyewe hivyo endapo wataonesha uzembe wa kupuuzia masomo ni dhahiri kwamba wataharibu malengo yao, hivyo wanatakiwa kushika elimu na si mambo mengine yanayoweza kuwasababisha wasifikie malengo yao ikiwemo kupata ujauzito.
Makete girls ni sekondari pekee na ni mpya ya wasichana iliyoanzishwa mapema mwaka huu wilayani hapo ambapo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 36
Na Edwin Moshi, Makete.