Mtakwimu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Bw. Vilerian Kidole akifafanua juu ya Umuhimu wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe Nchini kwa Wataalam kutoka kata za Hedaru, Makanya na Vunta wakati wa mafunzo yanayoendelea Hedaru, Wilayani Same juu ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa katika kata zao.
Mkuu wa Huduma za Hali ya Hewa kwa Jamii, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Bi. Hellen Msemo akisisitiza juu ya Umuhimu wa Kutumia Taarifa za Mamla ya Hai ya Hewa nchini katika Kupunguza Athari za Maafa kwa Wataalam wa kata za Hedaru, Makanya na Vunta (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Tarehe 25 Agosti, 2014, Hedaru, Wilayani Same (katikati) katika mafunzo yanayoendelea Hedaru, Wilayani Same juu ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa katika kata zao.
Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Jane Alfred akieleza jinsi jamii inavyoweza kukabili Maafa kwa Wataalam wa kata za Hedaru, Makanya na Vunta (hawapo pichani) katika mafunzo yanayoendelea Hedaru, Wilayani Same juu ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa katika kata zao.
Baadhi ya Wataalam katika Sekta ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu na Utawala wa kata ya Hedaru, Makanya na Vunta wakinukuu masuala muhimu katika mafunzo hayo yanayoendelea Hedaru, Wilayani Same juu ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa katika kata zao.