Sunday, August 31, 2014

MWANAAFA MWINZAGO AIBUKA KINARA WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014 NA KUONDOKA NA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA KITANZANIA



MWANAAFA MWINZAGO AIBUKA KINARA WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014 NA KUONDOKA NA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA KITANZANIA
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza akitoa neno kwa wadau waliojitokeza kushuhudia fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lililokuwa pia likirushwa live kupitia Kituo Cha Runinga cha ITV
Mwanaafa Mwinzago (katikati) akishangilia Mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kumsaka Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City na Kuhudhuriwa na Mamia ya Watanzania.
Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na wazazi wake na timu ya wafanyakazi wa TMT na washiriki wenzie mara baada ya kukabidhiwa mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Mara baada ya Kuwabwaga Washiriki wenzie tisa na Kuibuka Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kusaka Vipaji Vya Kuigiza Nchini lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limefikia Ukingoni Jana Katika Ukumbi wa Mlimani City.
Washiriki wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 waliofanikiwa kuingia Kumi Bora wakiwa wanasubiri mshindi atangazwe 
Host Wa TMT 2014 Joti akimpongeza Baba wa Mwanaafa Mwizago kwa Mwanae kuibuka Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) na kuibuka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Mwanaafa Akiwa amembeba Mdogo wake mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 na kuibuka na kitita cha Shilingi milioni 50.
Lulu akionyesha Bahasha iliyokuwa na JIna la Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) ambae ni Mwanaafa Mwinzago na Kumfanya kujishindia Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia fainali ya TMT ambayo ilikua ikirushwa live kupitia ITV.
Malaika Band wakitoa Burudani wakati wa fainali ya TMT 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo.
Christian Bella Akitoa burudani kwa kuimba wimbo wa Nani kama Mama ambao uliamsha Shamra Shamra katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo na Mwanaafa Mwinzago Kuibuka Mshindi.
Majaji wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 
Joti akitoa Suprize ya ukweli haswa katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) katika ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Proin Promotions, Geofrey Lukaza akiwa na Mkewe katika Red Carpet Kabla ya Show Kuanza katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia leo
 Mc Pilipili Akifanya Yake
 Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions Limited wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya MShindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) kupatikana na kila Mmoja kusherehekea Ushindi huo