Wednesday, August 27, 2014

MHE. LIBERATA MULAMULA AKUTANA NA MHE. ARNELL MILLS, MEYA WA MJI WA HELENA-WEST HELENA KUTOKA JIMBO LA ARKANSAS MAREKANI


MHE. LIBERATA MULAMULA AKUTANA NA MHE. ARNELL MILLS, MEYA WA MJI WA HELENA-WEST HELENA KUTOKA JIMBO LA ARKANSAS MAREKANI

Mhe. Meya Wills akipokelewa na Bw.Suleiman Saleh, Afisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Washington DC mara baada ya kuwasili Ubalozini hapo kwa mazungumzo na Mhe. Balozi Liberata Mulamula

Mhe. Liberata Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akiwa katika mazungumzo na Mhe.Arnell Wills, Meya wa mji wa Helena-West Helena, Arkansas, Marekani,Ubalozini Tanzania House, Washington DC.
Mhe. Balozi Mulamula akimkabidhi Meya Wills zawadi maalum kutoka Ubalozini.
.Mhe. Mulamula akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya Wills wa Mji wa Helena –West Helena, Arkansas, Marekani. 

Balozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula jana Jumanne Agosti 26, 2014, alikutana na Mhe. Mstahiki Meya wa Mji wa Helena-West Helena kutoka jimbo la Arkansas, Marekani, Ubalozini "Tanzania House" Washington DC. Mhe. Wills ambaye  Mji wake wake wa  Helena-West Helena una mahusiano ya kidada (Sister City) na Mji wa Moshi, Tanzania, alifika Ubalozini ili kufahamiana na Mhe.Balozi Mulamula pamoja na kumuelezea mashirikiano yaliyopo baina ya Mji wa Helena-West Helena na Moshi ambapo makubaliano rasmi yalisainiwa Oktoba 12, 2012, hapa Marekani kufuatia ziara ya Mhe. Japhary Michael, Meya wa Mji wa Moshi katika mji wa Helena –West Helena, Arkansas.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Wills alimuelezea Mhe. Balozi Mulamula juhudi zake katika kuimarisha mashirikiano hayo ya miji hiyo miwili ambapo yamejikita zaidi katika sekta ya utalii pamoja na shughuli nyingine za kukuza uchumi.

 Balozi Mulamula alimshukuru Meya Wills kwa kumtembelea na kufurahishwa na Meya huyo kutokana na kutembelea Tanzania mara mbili na kupata ufahamu zaidi wa Tanzania na hivyo kusaidia kupanua mahusiano yaliyopo baina ya Moshi na Helena –West Helena. Mhe. Mulamula alimshauri Mhe. Meya Wills kupanua wigo wa ushirikiano huo katika sekta nyingine za uchumi, biashara na uwekezaji.