1944 - URSULA SABINUS KWEKA - 2014
MAMA YETU, LEO UMETIMIZA MWEZI MMOJA TOKEA ULIPOITWA NA MUUMBA WETU HUKO JUU MBINGUNI. HATUNA SHAKA UKO NAYE KARIBU, NA IPO SIKU TUTAONANA TENA HUKO PARADISO. UKWELI UA ZURI LIMERUDI KWENYE BUSTANI YA EDEN.
TUNAKUKUMBUKA SANA KWA MENGI, HASA UVUMILIVU ULIOKUWA NAO, UKARIMU WAKO KWA WATU KATIKA SHIDA MBALIMBALI NA UPENDO, HAVITASAAULIKA MILELE. UKWELI UMEACHA PENGO KUBWA KATIKA FAMILIA YA MAREHEMU MZEE SABINUS KWEKA, TUMEBAKI WAKIWA MNO, LAKINI FARAJA TUZIPATAZO KWA WATU MBALIMBALI, ZINATUFUTA MACHOZI NA KUTUFANYA TUSIWE NA HUZUNI SANA .
UNAKUMBUKWA SANA NA MIMI MWANAO JANE, NA FAMILIA YOTE YA MZEE OTTO TINGO, KWA JINSI ULIVYOTUTUNUKU NA KUKAA NASI KWA KIPINDI KINGI CHA UGONJWA WAKO HADI MAUTI ILIPOKUKUKUTA, WANAO WENGINE WAPENDWA FESTO, EUGENIA, ELIZABETH, CECILIA NA THADEI AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE WALIKUUGUZA SANA KWA HALI NA MALI, WIFIYO WA PEKEE SR. DEVOTHA KWEKA CDNK, WAKWEZO DR. IBRAHIMU MSENGI, JOHN MUSHI, VALENTINA KINAWIRO, COSTANCIA MALLYA, FABIOLA FELICIAN, NA WOTE WA KWA TERRY, WAKE WENZIO PAULINA, LAWRENCIA, NA MONICA, WAJUKUU WOTE NA WOTE WA UKOO WA KWEKA NA CHAMI YA NARUMU POPOTE PALE WALIPO, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WOTE POPOTE PALE WALIPO.
RAHA YA MILELE UMPE Eee BWANA……………
WAKASAIDIANA KILA MTU NA MWENZAKE. KILA MTU AKAMWAMBIA NDUGU YAKE, `UWE NA MOYO MKUU`
ISAYA 41;6