Miriam Chirwa ndani ya makao makuu ya AU. |
Mnamo mwezi wa sita, kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, mtoto Miriam Chirwa alifanikiwa kuwakilisha watoto wa Tanzania kwa kuketishwa na wakuu, kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika, AU.
Miriam mwenye umri wa miaka 16, alifanikiwa kuwa mtoto pekee aliyeimba kwenye maadhimisho hayo, ambapo pia ni mtoto pekee aliyehojiwa na vyombo vya habari, akatoa ya moyoni.
"Napenda kuishukuru serikali ya Tanzania kwa kunipa heshima kuja hapa Addis Ababa kuwakilisha Taifa langu pamoja na watoto wote wa Tanzania katika siku hii ya mtoto wa Afrika. Pia nawashukuru kwa kunipa heshima ya kuongea kwa niaba ya watoto wenzangu.
Naomba viongozi wote wakuu dunia nzima waweke mkazo katika kutulinda watoto. Ndoa za utotoni zikomeshwe na adhabu zitolewe kwa wale wanaotumikishq watoto kwa njia zisizo sahihi. Watoto wenye vipaji wapewe fursa kushiriki mambo hata ya kitaifa kama hivi.
Hatma yetu watoto iko mikononi mwenu wazazi pamoja na viongozi. Asanteni kwa kunisikiliza"
Pamoja na kuzungumza na vyombo vya habari, Miriam alipata fursa ya kuimba wimbo wa Elimu ni Mwanga, na kisha kugawa albamu yake kwa watu kadhaa ikiwemo viongozi waliokuwa meza kuu.
Ulipitwa na habari hii, lakini sasa tumekufikishia.
Picha kwa hisani ya Edward Thomas.
Picha kwa hisani ya Edward Thomas.