Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia kwenye ukumbi wa NEC Dodoma ,akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana tayari kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC ,Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk.Maua Abeid Daftari akijadiliana jambo na mjumbe mwenzake Samia Suluhu Hassan muda mfupi kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa hakijaanza kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Oganizesheni Dk.Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Mjumbe wa Kati Kuu ya CCM DK. Salim Ahmed Salim ndani ya ukumbi wa mkutano wa White House kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakijadiliana kabla ya kuanza kwa kikao kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma, kutoka kushoto ni Profesa Anna Tibaijuka, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Dodoma.(Picha na Adam Mzee)